9.3 Je, ni nini kinachozuia rufaa kutolewa kikamilifu?

Kuna sababu nyingi za kutopata rufaa au rufaa hiyo kutotolewa kwa wakati unaofaa, ikiwa ni pamoja na:

  • Kutompa mama, baba na walezi wengine ushauri wa kutosha, ili waelewe uzito wa tatizo.
  • Umbali wa kituo cha afya na ukosefu wa usafiri.
  • Familia kukosa akiba ya pesa za usafiri.
  • Vituo vya afya havivutii baadhi ya wagonjwa. Mara nyingi, vituo hivi havina dawa muhimu na vifaa sahihi au havina wafanyikazi wenye ujuzi wa huduma zinazohitajika. Kwa sababu hiyo, wazazi wanaweza kusita kwenda katika vituo vya afya vyenye sifa mbaya.
  • Je, kuna chochote unachoweza kufanya kupunguza uwezekano wa kutofaulu kwa rufaa?

  • Rejela Kipindi cha 13 katika Moduli ya Utunzaji katika Ujauzito na majadiliano kuhusu Utunzaji Mahususi wakati wa Ujauzito. Kumbuka kuwa kupangia utunzaji wa dharura ni sehemu maalum ya ushauri ambao ungekuwa umetoa kwa kila mama mjamzito na familia yake kabla ya kuzaa. Familia inapaswa kuwa imeweka akiba ya pesa za safari na kupangia usafirishaji.

    Mwisho wa jibu

Pamoja na ushauri wa wakati wa ujauzito uliowafanyia kina mama wajawazito na familia zao, pia unahamasisha jamii kuhusika katika kuisaidia familia katika kipindi cha baada ya kuzaa. Kipindi cha 1 cha moduli hii kilijadili jinsi ya kutoa ushauri na uhamasisho ifaavyo. Kumbuka kuwa ni katika hali ya dharura unapoweza kuona kazi yako katika jamii ikizaa matunda.

  • Fikiria kuhusu mfano wa jinsi unavyoweza kurejelea jamii kwa usaidizi ukipata jambo la dharura baada ya mama kuzaa.

  • Pengine umefikiria mifano mingi tofauti. Ufuatao ni mfano mmoja tu. Familia haina pesa ya ziada na hawana mpango wa usafirishaji.Utamshawishi mtu wa aliye na gari kumpeleka mama na mtoto mchanga katika kituo cha afya kwa sababu wako katika hali ya kufa au kupona. Kwa msingi wa ulivyohusisha jamii hapo awali, unaweza kupata makubaliano ya mapema kutoka kwa viongozi wa kijiji kuwa pesa zitatolewa katika hazina ya jamii kulipia usafirishaji ikiwa familia haiwezi kuimudu. Unawashukuru viongozi wa jamii kwa usaidizi wao na utambuzi kuwa hali za dharura zinaweza kushughulikiwa vyema mara nyingi katika kituo cha afya cha ngazi ya juu ikiwa wagonjwa watafika katika muda unaofaa.

    Mwisho wa jibu

9.2.2 Kufahamu kuhusu vituo vya afya katika eneo lako

9.4 Jinsi ya kufanikisha rufaa