9.4.2 Usafirishaji na mpango wa dharura wa uhamishaji

Kwa kawaida, kila kijiji au jamii ina mfumo wao wa mpango wa dharura wa kuhamisha wagonjwa, ambao utaanza kufanya kazi mara moja haja inapotokea, kuna uwezekano wa kuhakikisha kuwa kuna usafirishaji uliotayari ili kuwezesha kina mama au watoto walio katika hali mahututi kufika katika kituo cha afya wakati ufaao.

  • Andika kwa haraka hatua mbili unazoweza kuchukua ukiwa na mama au mtoto anayehitaji kufikishwa katika kituo cha afya kupokea huduma maalumu.

  • Unaweza kuandika arifa ya rufaa na uwasaidie watu wa familia hiyo kupata pesa za kumsafirisha mama na mtoto hadi katika kituo cha afya kilicho karibu.

    Mwisho wa jibu

Ukishahakikisha kuwa mama na mtoto wamepata namna ya kusafiri, bainisha kama kuna usaidizi wa kutosha kwa watoto au watu wengine wa familia waliobaki nyumbani wakati mama na wahudumu wengine wameondoka.

Ikiwezekana, panga kuandamana na mama au mtoto mgonjwa hadi katika kituo cha afya.

Usipoweza hakikisha kwamba ameandamana na mtu mzima atakayewashughulikia kwa niaba yako. Kumbuka kumweleza mtu huyu kuwasiliana nawe mara tu atakaporudi kijijini, ili kujua kwamba mgonjwa alifika kituoni salama. Anaweza pia kukufahamisha jinsi mama au mtoto anavyotibiwa. Kama hajawasiliana nawe kwa siku moja au mbili, nenda nyumbani udhibitishe iwapo walirudi kutoka kituoni, na jinsi wanavyoendelea.

9.4.1 Utaratibu mwafaka wa kuweka stakabadhi

9.4.3 Kuhakikisha kuwa watu kituoni wanafahamu jinsi ya kuwasiliana nawe