9.4.3 Kuhakikisha kuwa watu kituoni wanafahamu jinsi ya kuwasiliana nawe

Wahudumu wa afya wa vituo vilivyo karibu wanahitaji kuangalia na kufahamu majina ya vijiji na maafisa wanaoendeleza elimu ya afya (au wahudumu wengine wa afya) walio katika vituo vidogo vilivyo karibu na kituo cha afya. Hakikisha kuwa wana habari yote wanayohitaji hasa kuhusu mahali wanapoweza kukupata, na njia bora zaidi ya kuwasiliana nawe. Iwapo utapata kuwa hawajakupatia habari yote unayohitaji wakati wanakutumia mgonjwa tena, wasiliana nao na uwaulize majibu yaliyoandikwa pamoja na utambuzi, kile tayari wamekifanya na unachohitajika kufanya. Wavutie kwa utaalumu wako na uhakikishe kuwa wanakutambua kama mmoja wa wahudumu wa afya wa thamani katika jamii.

Kwa njia nyingine, ili mfumo mzima wa afya uwe na ufanisi, wahudumu katika vituo vya afya vya ngazi ya juu na wale walio katika jamii wanahitajika kufanya kazi kwa pamoja. Ikiwa juhudi za kila mmoja zitaratibiwa, kuna nafasi nzuri ya kufikia lengo kuu - kuokoa maisha ya kina mama na watoto wachanga.

Kisha hatimaye, kila mtu angependa kuona maendeleo ya uboreshaji wa mfumo mzima kwa huduma ya afya. Njia moja ya kufikia lengo hili ni kupitia ukaguzi wa utendakazi mara kwa mara. Kuleta pamoja kila anayehusika ili kujadiliana jinsi unaweza kuboresha uratibu wa shughuli zako ili kufanya uendeleshaji wa huduma kuwa na mafanikio kwa wote wanaohusika.

9.4.2 Usafirishaji na mpango wa dharura wa uhamishaji

Muhtasari wa Kipindi cha 9