Somo la 2

Kuelewa tofauti katika mawazo na hisia za watu ni muhimu katika kukuza mahusiano mazuri. Ni muhimu unaposhughulika na kundi la vijana, kutoka miktadha tofauti (usuli na mazingira), lenye mawazo na hisia tofauti. Wanafunzi wako wanapaswa kuelewa hili ili liwasaidie wawasiliane kwa ufanisi na umakinifu.

Hata hivyo, kabla hatujaelewa mawazo na hisia tofauti, tunapaswa kwanza kuvitambua.

Unaweza kulinganisha mawazo ya watu kwa kupanga uchunguzi. Unahitaji kupanga namna ya:

  • kupanga uchunguzi;

  • kuufafanua kwa wanafunzi;

  • pima kama wameelewa.

Uchunguzi Kifani 2 na Shughuli 2 vinaonesha namna ya kufanya mambo haya, na Nyenzo-rejea 2: Kuuliza maswali kuhusu hisia inatoa mawazo juu ya namna ya kukusaidia katika upangaji wako.

Uchunguzi Kifani ya 2: Kutumia makundi kujadili mawazo na hisia

Wiki moja Bwana Kimaro alitumia uchunguzi wa ‘Je, unapenda…?’ katika darasa lake la III (tazama Shughuli 2). Alirekodi majibu na kuyabandika kwenye ukuta. Mara kwa mara, aliwakuta wanafunzi wanayasoma na kuyazungumzia.Wiki iliyofuata, Bwana Kimaro aliwauliza tena juu ya mambo wanayoyapenda na yale wasiyoyapenda, lakini safari hii, alichora sura mbili ubaoni:

MAMBO WANAYOYAPENDA MAMBO WASIYOYAPENDA (FURAHA) (HUZUNI)

Kwa kila swali, walihesabu idadi ya MAMBO WANAYOYAPENDA darasani na kuandika idadi chini ya uso a. Waliandika idadi ya MAMBO WASIYOYAPENDA chini ya uso b.

Alipoanza kuzungumzia hisia, aliandika ‘FURAHA’ juu ya uso a, na HUZUNI juu ya uso b. Katika vikundi, wanafunzi walitaja vitu ambavyo viliwatia furaha au huzuni. Kufanya kazi katika vikundi vidogo kulisaidia kushirikisha wanafunzi wakimya zaidi.

Alirudia zoezi, safari hii akitumia: HASIRA HOFU

Wakifanya zoezi katika vikundi vya wanne wanne au watano watano, wanafunzi walitaja vitu vinavyowakasirisha au kuwaogopesha. Walishirikiana kubadilishana mawazo muhimu pamoja kama darasa. Waliangalia kama baadhi ya vitu viko katika orodha zaidi ya moja na kujadili kwa nini hili limetokea. Bwana Kimaro alifurahishwa na jinsi wanafunzi walivyofikiri.

Shughuli ya 2: Uchunguzi kuhusu ‘Unapenda….?

Soma Nyenzo Rejea ya 3: Jinsi ya kuendesha uchunguzi darasani, na kujiandaa.

Labda uanze kwa kuwauliza wanafunzi wako maswali rahisi kuhusu vitu wanavyopenda na ambavyo hawapendi, kwa mfano

‘Wote mnapenda vitu vitamu?’ au ‘Mnapenda kazi za nyumbani?’

Katika vikundi vya wanafunzi wawili wawili, wafikirie maswali yao kuhusu vitu wanavyovipenda na ambavyo hawavipendi na kuviandika

Chora jedwali kutoka katika Nyenzo Rejea ya 3 ubaoni. Waambie wanafunzi walinakili na chagua maswali matatu kati ya yale waliyoyaandika. Kama darasa ni la ngazi ya juu unaweza kuweka maswali mengi zaidi.

Eleza kwamba wanafunzi wote watawauliza maswali wanafunzi watano na kuandika N au H chini ya majina yao.

Waambie wanafunzi katika vikundi walinganishe majibu yao. Waambie baadhi ya wanafunzi wasome kwa sauti maswali na majibu yao ili darasa zima lisikilize majibu tofauti. Jadili wamegundua nini kutokana na uchunguzi wao.

Fikiria wanafunzi wamejifunza nini kutokana na shughuli hii na jinsi ulivyoelewa jambo hilo.