Namba ya moduli 2: Kuchunguza Maumbo na Uwazi

Sehemu ya 1: Kuchunguza maumbo

Swali Lengwa muhimu: Unawezaje kuwasaidia wanafunzi kuendeleza na kutumia msamiati wa kihisabati kuhusu maumbo?

Maneno muhimu: kitu; umbo; jiometri; lugha; uainishaji; shughuli sifunge

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • umetumia shughuli za uchanganuzi sifunge ili kutalii maarifa ya maumbo;
  • umechunguza mbinu za kimatendo za kuwatambulisha wanafunzi lugha au ‘rejista’ ya istilahi za kihisabati;
  • umetumia shughuli za kimatendo kuendeleza uelewa wa wanafunzi na matumizi ya ufafanuzi wa msingi wa kihesabu wa maumbo ya kijiometri.

Utangulizi

Kugundua maumbo au kutalii jiometri na wanafunzi wako kunaweza kuwa shughuli yenye manufaa. Utumiaji wa mbinu ya utendaji na vitu vinavyotoka katika mazingira waishimo wanafunzi, vinaweza kusaidia kuhamasisha motisha na shauku.

Katika sehemu hii, unatumia vitu vilivyomo katika maisha ya kila siku ili kuwasaidia wanafunzi kukuza ujuzi muhimu za kijiometri, kama vile utambuzi, uundaji taswira akilini, utoaji maelezo, uchambuaji, kutaja, uainishaji na ulinganishaji.