Nyenzo-rejea ya 4: Uchunguaji wa wanafunzi
Taarifa za msingi/welewa wa somo kwa mwalimu
Uchunguaji au uangaliaji wa wanafunzi wako wakiwa wanafanya kazi darasani au wakiwa wanacheza uwanjani ni njia nzuri ya kuwatambua wanafunzi hao. Hali hiyo inakusaidia kujua wanashirikiana na nani au kutambua kama wanafunzi hao ni wapweke. Taarifa ya aina hiyo inaweza kukusaidia kupanga shughuli ambazo zinaendana na matakwa yao. Je, huzungumza zaidi katika vikundi ? Kama hivyo ndivyo, basi shughuli za kufanya katika vikundi, zinaweza kuwasaidia kufikiri zaidi na hivyo kujifunza zaidi.
Unaweza kutambua:
vikundi ya kijamii katika darasa lako na jinsi wanavyoshirikiana au wasivyoshirikiana. Kuna aina gani ya migogoro, kama ipo? Unawezaje kutumia maarifa haya kupanga kazi za vikundi ?
wanafunzi binafsi na stadi zao za kijamii, maslahi yao, n.k. Vipengele ambavyo unaweza kuchunguza wakati unapokuwa na
wanafunzi wako viko katika jedwali hapa chini. Lakini kumbuka kuwa mwangalifu zaidi na rekebisha maoni yako kwa kadiri unavyoendelea kuwajua zaidi wanafunzi wako.
Mifano hii hapa chini inaonesha jinsi ya kurekodi uchunguaji wa wanafunzi.
O = Hajishughulishi kabisa 1= Mbaya 2= Wastani 3= Vema
Hajishughulishi kabisa | Vibaya | Wastani | Vema | |
0 | 1 | 2 | 3 | |
a) Mwanafunzi anajishughulisha kikamilifu katika somo | ||||
b) Mwanafunzi ana uwezo wa ubunifu | ||||
c) Mwanafunzi anashiriki kikamilifu katika vikundi | ||||
d) Mwanafunzi anashiriki katika kutoa mawazo/taarifa kwa wenzake | ||||
e) Mwanafunzi anaonesha ushahidi wa kuelewa somo | ||||
f) Mwanafunzi haogopi kuuliza maswali | ||||
g) Mwanafunzi anaheshimu mawazo ya wenzake darasani |
Vyanzo vya asili: World Bank, Website
Nyenzo-rejea ya 3: Jinsi ya kuendesha uchunguzi wa darasa