Somo la 3

Katika sehemu ya kwanza ya sehemu hii, tumebainsha vipengele muhimu vinavyohitajika katika ukuaji bora wa kimwili. Sasa tunachunguza ni kwa vipi shule inaweza kutumia mawazo haya kwa wanafunzi na jamii husika.

Baada ya kujadili kwa kutumia mazoezi na michezo katika masomo yako, unahitaji sasa kuhamasisha kuhusu umuhimu wa a) chakula bora b) kujilinda kutokana na maradhi, na c) mazingira safi, lakini hili lazima lifanywe kwa umakinifu.

Hili linaweza kufanyika kwa kufanya shule kuwa mazingira yanayohamasisha kuhusu afya

Hili litahusisha majadiliano na wafanyakazi wa shule, kuhusu:

  • Kuiweka shule kuwa mfano mzuri kwa wanafunzi na jamii. Kufanikisha hili, unaweza kuhitaji kupanga na kuihusisha jamii na watu wengine kufanya kazi pamoja, kama vituo vya afya vilivyo kwenye makazi na Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs);

  • Kuhimiza mazoea ya kuishi katika hali bora katika shule yako kwa kuwa na shughuli zinazohamasisha afya kama ratiba ya kawaida ya kila siku.

  • Kupata mawazo kutoka kwa wataalamu kama waratibu wa UKIMWI na vituo vya afya.Nani atakayehusika, na wakati gani?

Uchunguzi kifani ya 3: Kuwa na siku ya Michezo ili kuhamasisha maendeleo ya afya

Baada ya kutumia michezo katika somo lake, Amani alifikiri kuhusu njia nyingine anazoweza kutumia kuendeleza afya katika shule.

Aliamua kuweka siku ya Michezo kwa shule na jamii. Mara moja kwa muhula, shule nzima inaweza kushindana katika michezo. Hii itahusisha michezo kama vile mpira wa miguu na kukimbia, lakini pia baadhi ya michezo ya kujifunza kama vile mmoja kuhusu alama za dira alizokuwa anatumia katia somo.

Katika kupanga hili, aliorodhesha watu atakaozungumza nao, kama vile mwalimu mkuu wa shule, walimu wengine, Chama cha Walimu na Wazazi (CWW) na wanafunzi.

Baada ya kuungwa mkono na mwalimu mkuu wa shule, alipanga mashindano na wafanyakazi wengine wa shule na CWW. Kwanza, waliamua kuhusu muda –yataanza saa 03.30 asubuhi na kumalizika saa 6.30 mchana. Kisha walichagua shughuli mbalimbali. Walipanga michezo na mashindano kulingana na madarasa, na kuandika ratiba ya shughuli kwa siku hiyo.

Halafu, walipanga ni nani atakayesaidia siku hiyo: CWW, Wajumbe wa Bodi ya Shule (WBS), walimu na baadhi ya watoto wakubwa Waliamua ni nani atatoa matangazo, atarekodi matokeo, atatoa zawadi, nakadhalika.

Kwa njia hii, walitengeneza ratiba nzima ya Siku ya Michezo. Walipanga kwa muda zaidi ya wiki mbili mpaka tatu, inaamisha kuwa ilipangwa vizuri na ilikuwa na mafanikio makubwa.

Soma Nyenzo–rejea 5: Mawazo mengine ya Amani kwa ajili ya kuendeleza afya kwa utambuzi zaidi.

Shughuli muhimu: Wigizo kifani kuhusu tofauti

Kwanza, jadili na wanafunzi wako , picha katika Nyenzo-rejea 6: Picha ya shule ambayo mazingira yake si bora, na waambie wabainishe matatizo katika mazingira ya shule hii.

Wapange wanafunzi wako kufanya uchunguzi katika mazingira ya shule yenu ili kuona kama shule inaboresha mazingira au inafifisha ubora wa mazingira. Watume wanafunzi wawili wawili au watatu watatu ili kuandika jambo lolote linaloendana na makundi haya katika mazingira ya shule.

Kisha, kila jozi/kikundi ki wasilishe waliyopata kwa darasa zima. Tengeneza orodha ya yale waliyopata na yaweke katika mabango mawili ukutani –moja kwa ajili ya uendelezaji bora wa mazingira na nyingine kwa ajili ya ushushaji wa mazingira bora. Jadili nini kifanyike ili kufanya mabadiliko kwa ajili ya mazingira bora ya shule. Kumbuka kushangilia vipengele chanya vya mazingira ya shule yenu.

Mwulize mwalimu wako mkuu wa shule kama unaweza kuwasilisha matokeo hayo kwa shule nzima katika baraza la shule. Mkaribishe kila mmoja hapo shuleni kuunda timu za kukabiliana na kazi zinazohitaji mabadiliko kufanya shule yenu iboreshe mazingira kikamilifu.

Unaweza kuwaambia wazazi na wanajumuiya wengine kusaidia. Pia, unahitaji kuwahimiza watoto kuwa wabunifu na kufikiri njia za kuimarisha mazingira ya shule bila kutumia gharama au fedha nyingi.

Nyenzo-rejea ya 1: Utangulizi wa Ukuaji wa kimwili