Nyenzo-rejea ya 1: Utangulizi wa Ukuaji wa kimwili

Taarifa ya msingi/Maarifa ya somo kwa mwalimu

Sote tunakua kila wakati. Tunakua kimwili, lakini pia mawazo na uelewa vinapanuka, na mara nyingi vyote hivi hutokea pamoja.

Kipindi cha miaka ambayo watoto wanakuwa shuleni, wanapitia mabadiliko mengi ya kimwili. Unaweza kuona mabadiliko haya kwa kuwalinganisha wanafunzi wa madarasa tofautitofauti. Watoto wenye umri mkubwa wanakuwa ni warefu na wenye nguvu zaidi, na kwa kawaida wanaweza kujieleza vizuri zaidi. Watoto pia wanakua kijinsia wanapofikia umri wa ujana, kuanzia miaka kumi na mitatu hadi ishirini, kama sehemu ya mchakato asilia.

Watoto hawawezi kuongezeka na kukua wao wenyewe. Kama mmea unavyohitaji maji, jua na afya nzuri ili kukua, vilevile watu wanahitaji vitu vya kuwasaidia. Vitu hivyo hujumuisha:

  • Chakula bora;

  • Mazoezi;

  • Kinga dhidi ya maradhi;

  • Mazingira safi.

  • Kila moja ya vitu hivi huchangia katika ukuaji wa kimwili wa mtoto

  • Kama mtoto hali vizuri, hatakua haraka kama wengine. Chakula huchangia pamoja na vitu vingine pia; kiasi cha nishati waliyonayo watoto, kiasi cha kinga dhidi ya maradhi n.k

  • Kama watoto hawafanyi mazoezi, misuli ya mikono na miguu yao haiitaimarika na hivyo hawatakuwa na nguvu. Mazoezi ya viungo pia yanasaidia kukua kwa viungo wakati wanapofanya mazoezi kama ya kukimbia, kuruka na kudaka. Kiungo husaidia katika stadi nyinginezo kama kusoma na kuandika. Mazoezi ya viungo ni mazuri kwa afya ya ukuaji wa kimwili.

  • Kama watoto hawakingwi dhidi ya maradhi, wataugua mara kwa mara ambako kutaathiri ukuaji wao. Kama watoto wanaumwa hawawezi kufanya mazoezi na hivyo misuli yao haitaimarika. Iwapo watoto wanaumwa wataona ugumu wa kusoma. Na hivyo watashindwa katika ujifunzaji wao.

  • Kama watoto hawana mazingira safi, wanakuwa rahisi kupatwa na magonjwa. Magonjwa yatawaathiri sawasawa na ambavyo maradhi yanavyowaathiri.

Ni muhimu kwako kuwatangulizia wanafunzi wako mawazo haya mapema kabisa ili wajenge tabia ya kuona kuwa afya ni sehemu ya maisha yao ya kila siku, lakini unahitaji uwe makini sana na muktadha wa jamii husika.

Nyenzo-rejea ya 2: Kupanga njia za kutoa utangulizi kuhusu kanuni nne za ukuaji wa kimwili.