Nyenzo-rejea ya 2: Kupanga njia za kutoa utangulizi kuhusu kanuni nne za ukuaji wa kimwili.

Taarifa ya msingi/ welewa wa somo wa mwalimu

Rejea Sehemu 1 ya moduli hii. Wanafunzi walikuwa wanalinganisha jinsi wanavyofanana na kutofautiana. Unawezaje kutumia zoezi hili darasani katika kutoa utangulizi wa kanuni nne za ukuaji wa kimwili?

Kwa mfano, ungeweza kuwaambia walinganishe umri wao na maumbo yao, pamoja na vyakula mbalimbali wanavyokula. Ili kumaliza kanuni nne za ukuaji na kimwili katika andalio la somo, fikiria maswali yafuatayo:

  • Kitu gani muhimu unachotaka wajifunze?

  • Utatoaje utangulizi wa mada?

  • Utapangaje kazi? Maelekezo yako yatakuwa yapi? Je, wanafunzi watafanya kazi katika vikundi au wawili wawili?

  • Utaoneshaje zile kanuni nne?

  • Ungetumia nyenzo-rejea zipi katika kusaidia kuzieleza? Kwa mfano, ungeweza kutumia picha? Ungeleta aina zipi za vyakula? Ungevipata wapi?

  • Utapimaje welewa wa mwanafunzi?

  • Mambo gani ambayo unatakiwa uwe makini nayo?

Andika majibu yako ya maswali haya kwenye karatasi kisha yatumie katika kupanga kila hatua ya somo lako. Daima kumbuka kuwa makini na muktadha husika ili usiwaudhi wanafunzi.

Nyenzo-rejea ya 1: Utangulizi wa Ukuaji wa kimwili

Nyenzo-rejea ya 2: Kutumia michezo na mazoezi ya viungo