Nyenzo – Rejea 4: Jinsi Amani alivyofundisha somo lake

Taarifa ya msingi/welewa wa somo wa mwalimu

Hapa pana hatua alizotumia Amani katika somo lake:

  1. Kwa kutumia kazi ya vitu `vipendwavyo’ na ‘visivyopendwa’ iliyoelezwa katika sehemu 1 ya moduli hii, kila mtu aliandika michezo mitano anayoipenda zaidi.
  2. Amani aliwaambia wanafunzi wazungumze, wawili wawili, kuhusu michezo wanayopendelea na kuchagua mchezo mmoja kati ya michezo hiyo. Zoezi hili lilichukua dakika kumi.
  3. Kufanya uchunguzi, alisimama mbele ya darasa akikiuliza kila kikundi ni mchezo gani waliouchagua.
  4. Aliandika mchezo huo ubaoni na kuweka alama ya vema pembeni yake. Kama ni mchezo ambao umeshachaguliwa na mtu mwingine, aliongeza tu alama ya vema. Orodha ubaoni ilionekana hivi:

Mpira wa miguu √ √ √ √ √ √

Kuruka kamba √ √ √ √ √ √ √

Kukimbizana/kuvuta kamba √ √ √ √ √ √

Kudaka √ √ √ √

Gololi √ √ √

  1. Usawiri ulichukua dakika 15 kumalizika. Baadaye, aliuliza ni mchezo upi uliozoeleka/uliofahamika zaidi na ambao haukuzoeleka/haukufahamika sana.
  2. Aliliambia darasa liunde makundi saba ya watu watano watano. Aliliambia kila kundi lichague mchezo mmoja na kuandika maelezo ya jinsi ya kuucheza.
  3. Aliwaambia wasome maelezo/maelekezo yao darasani.

Kulikuwapo na michezo mingi sana ya kuelezea kwa somo moja hivyo aliamua kushughulikia mchezo mpya mmoja mmoja wakati wa somo la mwisho la kila siku.

Katika kusaidia hili, alilipatia kila kundi jina lkutokana na siku za wiki. Sasa kila kundi lilifahamu ni lini lingetoa maelezo yake. Kila siku ilipoanza, aliuliza ilikuwa zamu ya nani ya kutoa maelezo.

Masomo haya yalitumia mpangilio ufuatao:

  1. Kwanza, kila kundi lilitoa maelezo ya mchezo na kuuonesha mbele ya darasa lote. Hii ilichukua kama dakika kumi;
  2. Kisha makundi yote yalifanya mazoezi ya kuucheza huo mchezo pia. Kama ni muhimu Amani aliwapeleka nje. Hii ilichukua dakika 15.
  3. Baadaye, aliwaambia wafikirie njia mpya za kuucheza mchezo huo kwa lengo la kuwasaidia kukumbuka kile walichojifunza darasani kwa siku hiyo.
  4. Kila kundi lilikuja na mawazo mapya kwa ajili ya kuurekebisha mchezo. Mjadala huu kwa kawaida ulichukua takribani dakika 15.
  5. Mwisho, walijadili baadhi ya mabadiliko na kuyafanyia majaribio kwa pamoja mpaka somo lilipokwisha.

Kwa njia hii, Amani alianza kutumia michezo ya wanafunzi wake katika kusaidia kufundisha masomo mbalimbali. Mawazo mazuri aliyatumia tena. Pia, wanafunzi walianza kucheza michezo mipya kwa kujifunzia wakati wote wa mapumziko.

Nyenzo-rejea ya 2: Kutumia michezo na mazoezi ya viungo

Nyenzo – rejea 5 Mawazo mengine ya Amani kwa uhamasishaji wa Afya