Nyenzo – rejea 5 Mawazo mengine ya Amani kwa uhamasishaji wa Afya

Taarifa ya msingi/welewa wa somo kwa mwalimu

Kama ilivyokuwa Siku ya Michezo, Amani alikuja na mawazo mengine ya kuhamasisha afya shuleni, kama vile:

  • Wanafunzi na walimu wangeweza kusafisha uwanja wa michezo na madarasa baada ya kusanyiko la kila asubuhi.

  • Utumiaji wa mapipa ya takataka kungeweza kuwafanya watu waache kutupa takataka kila mahali (kungeweza kuwazuia mbwa na panya kuja shuleni na kupunguza uwezekano wa watoto na walimu kushambuliwa na magonjwa na kuugua).

  • Kutumia shule kama kituo cha chanjo wakati wafanyakazi wa afya wanapoitembelea kungekuwa na uhakika kwa watoto na walimu kupata chanjo ya mara kwa mara. Pia kungesaidia watoto kupata miongozo ya afya kutoka kwa madaktari na wauguzi.

  • Kuanzishwa kwa mahusiano kati ya shule, wenyeji na wafanyakazi wa afya kungesaidia shule kupata nyenzo za afya.

  • Kuendeleza bustani ya shule kungesaidia kwa chakula (kama vile mboga za majani kwa ajili ya kutengenezea supu) na mazoezi, na pia kujifunza kuhusu mazingira.

  • Eneo au chumba cha huduma ya kwanza au cha kupumzikia kingeweza kuanzishwa.

  • Shule ingeweza kuwaalika wageni kuja kuzungumzia kuhusu matatizo mahsusi kama vile VVU/UKIMWI, Malaria, n.k.

  • Wangeweza kuendesha mazoezi baada ya kutoka shuleni au vilabu vya michezo.

Nyenzo – Rejea 4: Jinsi Amani alivyofundisha somo lake

Njenzo –rejea 6: Picha ya shule yenye mazingira duni kiafya