Sehemu ya 3: Kuchunguza mawazo ya wanafunzi juu ya kuishi kiafya

Swali Lengwa muhimu: Unawezaje kutumia maarifa yaliyopo na kazi za vikundi kukuza welewa wa kuishi kiafya?

Maneno muhimu: majadiliano ya vikundi; kusimulia ngano; kuandika; mazoea ya kiafya ya kijadi; maarifa yaliyopo

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • Kutumia majadiliano ya darasani na vikundi kutambua mambo ambayo wanafunzi wanajua;

  • Kujifunza jinsi ya kuongeza maarifa waliyo nayo wanafunzi; 

  • Kutumia wawezeshaji wenyeji kuhamasisha wanafunzi kujifunza.

Utangulizi

Unapoingiza somo la kuishi kiafya katika mtaala wako, unahitaji kuwa makini na mazingira ambamo utafundishia. Sehemu hii inajumuisha uchunguzi wa maarifa ambayo wanafunzi huwa nayo kabla ya mafunzo – wanapopata mawazo yao na maarifa wajayo nayo darasani –na kuyatumia kukuzia fikira zao juu ya kuishi kiafya. Kwa kutambua maarifa ya wanafunzi wako na umahiri wao, utajenga kujiheshimu kwao.

Shughuli zinakutaka utumie majadiliano ya vikundi, kazi za vitendo na wenyeji kutalii na kuimarisha ujuzi wa wanafunzi wako juu ya kuishi kiafya.

Njenzo –rejea 6: Picha ya shule yenye mazingira duni kiafya