Somo la 1

Wanafunzi wako wanatakiwa kufahamu vyakula gain ni bora kwao, lakini kuwaambia tu haitoshi. Hapa, tutachanguza njia shirikishi zaidi ili kuwasaidia kujifunza na kuelewa.

Jambo muhimu ni kwamba, wanafunzi wanaweza kuwa tayari wana mawazo fulani kuhusu mada hii. Kutafiti mawazo hay ani yapi, unaweza kuanza somo lako kwa:

  • kuanzisha mada kwa kuwauliza ‘Mnaweza kuniambia nini kuhusu…’ na kuandika mawazo yao;

  • kuwapanga wawiliwawili au vikundi vidogovidogo wazungumzie mada na kuwapa maswali yasiyo na mpaka kuongoza majadilaino yao;

  • kuwataka wajibu, na kuorodhesha mawazo muhimu unayotaka kufuatilia.

Baada ya kujua maarifa waliyo nayo wanafunzi wako, upangaji wako –na ufundishaji wako –utaoana na mahitaji yao. Tazama Nyenzo-rejea muhimu: Kutumia maswali kukuza kufikiri itakayokusaidia kufikiria maswali ya kuongoza majadiliano yao.

Uchunguzi kifani ya 1: Kutafiti wanafunzi wanajua nini juu ya lishe nzuri

Bibi Shivute, wa Shule ya Msingi ya Tabora Tanzania, aligundua kuwa darasa lake lilipenda kuzungumzia chakula; kwa hiyo, aliwataka wanafunzi waorodheshe vyakula vyote wanavyovipenda.

Aliwauliza vyakula hivyo –mimea na wanyama -vilitoka wapi mwanzoni. Katika vikundi, walikata picha za vyakula toka kwenye magazeti ya zamani ambayo Bibi Shivute alikuwa amekusanya na kuyahifadhi darasani kwake; kisha wakayapanga katika makundi mbalimbali ya vyakula (tazama Nyenzo-rejea 1: Mazoea ya Kuishi Kiafya ).

Walijadiliana aina za vyakula ambazo ni za manufaa kwa mtu na zile ambazo zinaweza kuwa na ladha nzuri lakini si za manufaa.

Bibi Shivute alizungumzia vyakula vingine ambavyo hawakutaja, na aliwataka waviingize katika mpangilio wao. Alielezea kuhusu kula mlo kamili kama inawezekana, na kula matunda na mboga zaidi, na kupunguza utumiaji wa sukari. Watoto walichora picha za vyakula hivyo mbalimbali.

Aliwauliza kama wanafahamu kwa nini nyama na samaki vina manufaa kwao. Walikuwa namazwazo mengi: mvulana mmoja alisema kuwa nyama na samaki huwasaidia watoto kukua. Bibi Shivute alifurahi sana, na kuwaeleza jinsi vyakula hivi vinavyojenga misuli yao.

Walijadili ukweli kuwa fedha ni tatizo; hawana budi kula chakula ambacho wazazi wao wanakimudu na mara nyingi si chakula wanachotaka kula na wala si kile chenye manufaa kwao. Walitambua kuwa heri kupata chakula chochote kuliko kutopata kabisa.

Shughuli ya 1: Shughuli za makundi ya vyakula

Kabla ya kuanza, unaweza kupenda kusoma Nyenzo-rejea 1 .

  • Waulize wanafunzi wanataka kula nini. Wanaweza kuchora picha au kutafuta picha katika magazeti ya zamani kama unayo.

  • Watake wanafunzi, katika vikundi vidogovodogo, wabadilishane mawazo juu ya aina za vyakula ambavyo ni bora kwao kuliko vingine.

  • Kitake kila kikundi kitoe wazo moja na uyaorodheshe mawazo hayo ubaoni.

  • Kwa kutumia mawazo yao kama kianzio, eleza makundi mbalimbali ya vyakula na jinsi kila kundi linavyotusaidia. Tazama Nyenzo-rejea 3: Vyakula vya Kienyeji kwa ajili ya picha za vyakula ambavyo ni vya kienyeji zaidi kwa matumizi katika shughuli hii.

  • Watake wanafunzi, katika vikundi vyao, kuoanisha picha na makundi ya vyakula. Watake wajadiliane kwa nini vyakula mbalimbali vina manufaa kwao na vina manuufaa gani.

  • Kitake kila kikundi kuandika maswali matano juu ya aina mbalimbali za vyakula. Fanyeni zoezi la darasani –vikundi viulizane na kujibu maswali kwa zamu.

  • Mwishowe, vitake vikundi kuandaa mabango au makaratasi ya kubandika kwa kutumia michoro au picha zao. Unaweza pia kutumia sampuli au paketi tupu za vyakula. Hivi uviache darasani kwa ajili ya kuonwa na wote. ( Tazama Nyenzo-rejea 2: Mawazo kwa ajili ya makaratasi ya kubandika darasani)

Sehemu ya 3: Kuchunguza mawazo ya wanafunzi juu ya kuishi kiafya