Somo la 1

Michezo ni shughuli ya utendaji ambayo wanafunzi wanaweza kushiriki, kama burudani au kama njia ya kujifunza. Ni njia mojawapo pia ya kufundisha wanafunzi namna ya kushirikiana –kubadilishana mawazo na vielezo. Kushirikiana ni jambo muhimu shuleni kwa sababu:

  • shule nyingi zina vifaa vichache, na wanafunzi wanahitaji kutumia vifaa katika makundi;

  • wanafunzi wana stadi tofauti, kushirikiana kunahimiza kusaidiana;

  • kuhimiza kushirikiana na kazi za pamoja ina maana kuwa kila mmoja anajifunza hata kama hutamfikia kila mwanafunzi wako kipekee;

  • ushirikiano ni sehemu ya maisha na sote tunahitaji kushirikiana kila siku;

  • watu hujifunza namna ya kusaidia watu wengine na kuomba msaada inapotakikana kwa kushirikiana; na

  • ushirikiano ni njia mojawapo ya kuwa na marafiki na inahimiza mwingiliano wa kijamii.

Sehemu hii inachunguza njia mbalimbali za kushirikiana na jinsi unavyoweza kuhimiza ushirikiano kama sehemu ya ufundishaji wako wa kila siku.

Uchunguzi kifani ya 1: Njia mbalimbali za kushirikiana

Kembabasi ni mwalimu wa darasa la 4 katika shule mojawapo ya msingi kaskazini mwa. Ana wanafunzi wengi darasani mwake lakini ana vitabu vichache, daftari chache, na penseli chache. Kwa hiyo kwa kila somo la kusoma au la kuandika, anawaweka wanafunzi wake katika makundi ili kusaidiana vifaa hivyo ambavyo ni vichache. Anapanga utaratibu wake ifuatavyo:

  • Kila kundi linakuwa na kitabu kimoja, daftari moja na kalamu moja;

  • Katika kila kundi, mwanafunzi mmoja anakuwa na kitabu na husoma kwa sauti kwa wenzie, au husoma kwa zamu kila mmoja akisoma kipengele kidogo;

  • Mwanafunzi mmoja anakuwa na daftari na huandika majibu;

  • Wanafunzi waliobaki hujadili maswali na majibu yake;

  • Wote hukagua kilichoandikwa; na

  • Wanabadilishana nafasi kwa kila tendo wanalofanya.

Kabla ya darasa kuanza tendo la kusoma na kuandika, Kembabasi huuliza kila kundi ni nani atasoma na nani ataandika. Kwa njia hii, mwalimu huyu huhakikisha kuwa kila mwanafunzi hufanya zoezi la stadi ya kusoma, kuandika na kujadiliana kwa kadri inavyowezekana.

Wanafunzi hujifunza jinsi ya kusikilizana na kushirikiana katika kutoa mawazo. Wanapata maarifa kutokana na wao kwa wao na jinsi ya kuwa marafiki.

Kembabasi hubadilisha makundi mara kwa mara, na hivyo wanafunzi hukuza vipaji vipya na kupata marafiki wapya.

Unaweza kupata mawazo ya ziada kutoka katika nyenzo rejea muhimu:

Teaching in challenging environments ..

Shughuli ya 1: Mchezo wa kushirikiana

Huu ni mchezo unaohimiza lugha na ushirikiano

  • Gawanya darasa lako katika makundi matatu

  • Mpe kila mwanafunzi katika kundi la kwanza kadi iliyoandikwa kiwakilishi (k.v. mimi, wewe, yeye, sisi, wao)

  • Mpe kila mwanafunzi katika kundi la pili kadi iliyoandikwa kitenzi (k.v. taka/hutaka, nenda/huenda, kula/hula n.k.)

  • Mpe kila mwanafunzi katika kundi la tatu kadi iliyoandikwa jina/nomino (k.v. mpira, nyumba, embe n.k.)

  • Mwambie kila mwanafunzi kuwa lazima waunde sentensi kwa kuwatafuta wanafunzi wenzao na kushirikiana nao kwa kutumia maneno yao (k.m. hupenda kucheza mpira)

  • Kisha waulize wana makundi kuhakikisha usahihi wa sentensi

Unawezaje kubadilisha zoezi hili ili kufundishia masomo mengineyo, k.m. hisabati au sayansi?

Mtazamo huu unaoweza kubadilishwa unaweza kutumika katika mada mbalimbali.

Sehemu ya 4: Vitendo vya kuimarisha ustawi wa kisaikolojia