Somo la 2

Ukiwa mwalimu, majukumu yako makuu ni pamoja na kuwatia moyo na kuwasaidia wanafunzi wako kama wajifunzao na kama watu.

Mtaalamu wa Elimu ya Saikolojia aitwaye Maslow alibainisha mahitaji muhimu ya kisaikolojia yanayosaidia kujifunza vyema, ambayo ni:

  • Usalama na amani;

  • Mapenzi na kukubalika

  • kujithamini

Kila mwanafunzi ana tamaa ya kufanya vizuri, hali ambayo inaweza kupimika kwa kuzingatia jinsi mwanafunzi anavyojiheshimu. Wanafunzi wanaonesha hali hiyo darasani kwa kuwa makini katika kujibu maswali. Wanapojihisi wajinga wanaharibikiwa hali yao ya kujithamini na wanakata tamaa.

Lakini ukiwaonesha kuwa majibu yao yanaweza kuwa sahihi au ni ya mvuto, hali hiyo inaongeza moyo wa kujiheshimu na inatia moyo wa kushiriki kwao na kupata mafanikio.

Unaweza kuhimiza hali hiyo darasani kwa kuwa mwalimu thabiti na mwenye kutia moyo (positive and affirmative teacher). Maana yake ni:

  • kuwatia moyo na kuwaheshimu kunawafanya wanafunzi wajiamini na wachangie mawazo yao.

  • kuhakikisha kuwa hakuna mwanafunzi yeyote anayefanywa kujihisi mjinga au kuaibika wakati wa kuchangia mawazo yao.

  • kuhakikisha kuwa kila mmoja anaelewa kiini cha somo.

Ili kufanikiwa katika hili inakubidi utengeneza mbinu za ufundishaji ambazo hazikatai jibu litolewalo na mwanafunzi yeyote, bali utumie majibu ya wanafunzi katika kuwaelekeza kufikiri kwa kina zaidi. Kwa kufanya hivi, utakuwa unaimarisha moyo wa wanafunzi wa kujithamini.

Uchunguzi kifani ya 2: Kuwa mwalimu thabiti na mwenye kutia moyo

Mwalimu William Nyiru ameweza kuwahimiza wanafunzi wake wa darasa la II kutoa maoni yao katika masomo kwa kushirikiana katika shughuli mbalimbali kama mbinu mojawapo aitumiayo katika ufundishaji wake. Wanafunzi walianza kwa kuchangia katika makundi madogomadogo, na mwishowe walianza kujiamini na kuchangia mbele ya darasa zima.

Ili kuhakikisha kuwa hawavunji wanafunzi wake moyo wa kujithamini, alipanga jinsi ya kukabili mchango wao.

  • Aliwauliza wanafunzi wote darasani swali. Kama wanafunzi walipenda kujibu basi iliwabidi wanyooshe mikono na alimchagua mmojawapo kujibu.

  • Kama walijibu kwa usahihi mara moja, basi alikuwa akiwasifia kwa maneno kama ‘Umejibu vizuri!’ ‘Vizuri sana!’, ‘Vizuri sana sana!’

  • Kama wanafunzi walitoa jibu ambalo halikuwa sahihi kabisa, alikuwa makini kwa kutosema ‘Hapana’ au ‘Sio sahihi’. Badala yake alisema

  • ‘karibu umepata’ au ‘bado kidogo’. Angemshauri mwanafunzi ‘kujaribu tena’ na kuwapa dokezo au kuwashawishi wafikirie zaidi.

  • Kama mwanafunzi alishindwa kabisa, Mwalimu Nyiru aliendelea kwa kusema: ‘Nani anaweza kutusaidia?’

Kwa kadri walivyoendelea aligundua jinsi walivyojiamini zaidi.

Shughuli ya 2: kujenga moyo wa kujiheshimu

Njia mojwapo ya kujenga moyo wa kujiamini ni kuwasaidia wanafunzi kutambua stadi zao.

  • Waombe wanafunzi wako waeleze vitu/shughuli wanazofurahia kufanya, wakiwa nyumbani na shuleni.

  • Waulize ni shughuli zipi ambazo wana uwezo wa kuzifanya.   

  • Watenge kwenye makundi. Halafu muulize kila mwanafunzi aeleze stadi tatu maalum na awaelezee wenzake katika kundi.

  • Waulize mmoja mmja kwa wakati wake kuandika juu ya stadi hizi na wachore picha zao wakiwa wanafanya shughuli hizo. Wazitundike picha hizo kwenye ukuta.

Katika somo linalofuata, endeleza jambo hili kwa kuwauliza wanafunzi wako kuelezea watapenda kuwa nani au watapenda kufanya nini wakati

  • watakapokuwa watu wazima.