Somo la 3

Tumekwisha zungumzia jinsi ya kuwasaidia wanafunzi kutambua na kuelezea hisia zao. Kwa kuwa hisia ni akisi muhimu ya kutambua sisi ni nani kama watu binafsi, hisia hizo pia zinaweza kutufanya kuonesha hisia ambazo hatuwezi kuzizuia wakati wote.

Hisia zetu na tabia zetu vinaoanishwa na vitu viwili:

  • Hali halisi tuliyomo; na

  • Kuathirika kwa hisia zetu kunatokana na hali halisi hiyo, na uelewa wetu wa lipi hukubalika katika jamii katika kuonesha hisia zetu.

Kwa mfano, mmojawapo wa wanafunzi wako anaweza kufurahi kupita kiasi. Tendo lako la haraka labda litakuwa ni kuchukia. Lakini ukionesha hali hiyo utaharibu hali ya utulivu.

Ili kurekebisha hali hiyo, utamuomba akae chini kimya, au utampa shughuli ya kufanya kama vile kugawa vitabu ili umuondoe katika hali ile (ya kufurahi kupita kiasi).

Wanafunzi vijana huchukua muda mrefu kuelewa hisia zao na kanuni za jamii ambazo hutuelekeza jinsi ya kujiheshimu. Tunapokuwa wadogo, mara nyingi tunapitia katika mazingira ya hisia kwa mara ya kwanza na huwa hatujui jinsi ya kukabiliana na hali hiyo. Tunapokuwa watu wazima, tunajifunza kuelewa hisia zetu vizuri zaidi, na kudhibiti jinsi tunavyotenda katika mazingira tofauti.

Katika sehemu hii, tutaangalia jinsi ya kulihimiza jambo hili darasani.

Uchunguzi kifani ya 3: Kusaidiana

Mama Kweli alianza kufanya kazi na wanafunzi wake wa darasa la II ili kuwasaidia kuelewa zaidi kuhusu hisia na tabia zao- ni kitu gani kinawafanya kufurahi, kuhuzunika, kukasirika na kuogopa.

Baada ya kazi hiyo, pamoja na wanafunzi wake alitayarisha kazi kwa kutengeneza orodha ya vitu ambavyo wangevifanyiana ili kufurahi na sio kuhuzunika, kukasirika au kuogopa.

Wakiwa katika makundi na darasa zima, wanafunzi walitengeneza chati ya kanuni za kushirikiana wakiwa shuleni. Kanuni hizo zilihusisha vitu kama: ‘Kila siku tutaamkiana asubuhi’ na ‘ Hatutaitana majina mabaya’. Walihusisha kila kanuni pamoja na hisia kwa kuchora picha yenye kuonesha uso wa furaha au huzuni pembezoni mwake.

Kwa kutumia chati hii, Mama Kweli alirejelea katika kanuni za tabia wakati wote palipotokea tatizo la tabia (mbaya) darasani. Wakati wote alihusisha tabia na hisia tofauti iliyotokana na tabia hiyo.

Kwa njia hii, wanafunzi wake waliweza kuhisi tabia zao na hisia za watu wengine. Walianza kuwa waangalifu baina yao kutokana na matokeo haya.

Shughuli muhimu: Kutafakari kuhusu tabia yako (kujitafakari)

Katika shughuli hii, unaombwa kufikiria kuhusu tabia yako mwenyewe na kupanga jinsi ya kuidhibitisha na kuitegemeza katika darasa.

  • Kwanza, jiulize maswali yaliyoorodheshwa katika Nyenzo-rejea 1: kutafakari kuhusu tabia yako.

  • Andika majibu ya maswali hayo.

  • Zingatia chunguzi-kifani tulizoonesha katika sehemu hii. Chagua mojawapo

  • kutoka katika kila chunguzi ambayo unaweza kuitumia katika mazingira yako

    • ya ufundishaji.

  • Andika maelezo ya jinsi utakavyoitumia katika darasa lako.

  • Mwishowe andika mpango ‘wa utekelezaji’. Andika sentensi tano ukieleza tabia njema utakayotumia kila siku; k.m. ‘Nitwasalimu wanafunzi wangu wote nitakapowaona katika uwanja wa michezo’.

  • Zingatia Nyenzo-rejea 2: Tafakari ya mtazamo wa mama Msekwa. Ili kuuona mtazamo huo mwalimu mmoja alifundisha badala yake.

Nyenzo-rejea ya 1: Kutafakari juu ya tabia yako/Kujitafakari tabia