Nyenzo-rejea ya 1: Kutafakari juu ya tabia yako/Kujitafakari tabia

Usuli/maarifa ya somo kwa mwalimu

Kwa kutumia maswali yaliyopo chini, jifikirie tabia yako kama mwalimu. Uwe mkweli katika majibu yako. Kuna mifano kutokana na shughuli za darasani mwako ambazo zinathibitisha maoni yako?

  • Wewe ni mwalimu unayesaidia/usiyesaidia wanafunzi wako? Unawezaje kuwa wa msaada zaidi?

  • Unajaribu kuwatia moyo au kuwakatisha tamaa? Kwa vipi? Unawezaje kuwatia moyo zaidi?

  • Unawafanya wawe na furaha wanapojifunza? Kwa vipi?

  • Unawahuzunisha, unawakasirisha au unawaogopesha? Vipi?

  • Ni kipengele kipi cha ufundishaji wako unachohitaji kubadilisha? Utafanyaje?

  • Ni vipengele gani vya tabia za jamii za wanafunzi wako unazohitaji kubadilisha? Utawasaidiaje wanafunzi waweze kutimiza lengo hili?

Nyenzo-rejea 2: Tafakuri ya mama Msekwa kuhusu mkabala wake