Somo la 1

Tabia yako uwapo shuleni inaweza kuwaathiri wanafunzi wako kitabia na hamasa ya kujifunza kwa njia chanya au hasi. Aidha hali ya wanafunzi washirikianavyo pia inaweza kuleta athari hiyo. Tumekwisha jadili njia mbalimbali ambazo zinaweza kuwahimiza wanafunzi wako kufikiria hisia za kila mmoja wao. Katika sehemu hii tunazungumzia zaidi jinsi ya kuwasaidia wajione huru na salama. Katika hali hiyo watajifunza kwa ufanisi zaidi.

Kila mmoja hujitahidi kuwa huru na salama. Watu hujenga majumba yenye kuta, madirisha, na milango minene katika sehemu nyingi, ili wawe salama ndani ya majumba yao. Watu wengine huajiri walinzi kulinda nyumba na magari yao. Na wengine hupita huku na kule wakilinda mali zao wakiwa na silaha. Lakini vitu hivi hutulinda kimwili. Kama tulivyoona, watu hujihisi salama wakati wanapokuwa wamezungukwa na watu wanaowaamini. Njia nzuri ya kuhisi usalama huu ni kuwa na mtandao wa marafiki na wenzi wetu. Wanafunzi hawawezi kujifunza kwa uthabiti wakati wanapojihisi kutokuwa salama, au kuwa na wasiwasi.

Uchunguzi kifani ya 1: Kwenda shule katika hali salama

Siku moja, mwalimu Thuku wa darasa la tatu katika shule za Tanzania, alimkuta mwanafunzi mmoja mwenye wasiwasi akiwa pamoja na wenzie huku akilia. Rafiki zake walikuwa wakimfariji kwa kutumia lugha waliojifunza kuhusu namna ya kuwasiliana kuhusu hisia huku wakimuuliza tatizo lake.

Baada ya muda, mwanafunzi huyu aliwaeleza kuwa wakati akija shule alikutana na wanafunzi wakubwa watatu waliomtishia kumpiga na kunyang’anya begi lake la shule na viatu. Aliwakimbia ili ajifiche shuleni.

Kwa kusaidiwa na wanafunzi wengine, Mwalimu Thuku alimbembeleza na kumfariji kwa kumhakikishia kuwa alikuwa salama. Walimweleza kuwa kwa sasa alikuwa shuleni na wale wanafunzi waliomtishia wasingeweza kuja shuleni. Aidha walimweleza kuwa sasa alikuwa na mwalimu wake, na mwalimu huyo angewafukuza wanafunzi wote waliotaka kumsumbua. Alikuwa amezungukwa na marafiki; na wangemkinga.

Baada ya shule marafiki zake walimsindikiza hadi nyumbani na walizungumza na familia yake na majirani kuhusu yaliyotokea.

Siku iliyofuata, mwalimu Thuku aliamua kukutana na wanafunzi wake tena ili kujadiliana zaidi kuhusu usalama na jinsi ya kusaidiana.

Shughuli ya 1: Kujihisi salama – majadiliano

Tayarisha majadiliano kuhusu kuwa salama na kuwa na amani. Anza kwa kuelezea tukio lililompata mwanafunzi wa kiume kama ilivyojadiliwa katika sehemu ya uchunguzi kifani.

  • Waulize wanafunzi katika makundi yao madogo, waeleze hali ya nyumbani au shuleni wakati walipojisikia a) kuwa salama na kuwa na amani, na b) kutokuwa salama;
  • Wewe pamoja na darasa zima, bainisheni baadhi ya mawazo yanayohusu hali tunayohisi kuwa salama na kutokuwa salama. Orodhesha mawazo hayo ubaoni;
  • Watake wanafunzi kujadili wangefanya nini kumfanya kila mmoja kujihisi salama darasani na katika uwanja wa michezo; na

Mwishoni, orodhesha ubaoni tabia zinazofanya wanafunzi wajihisi salama darasani na katika uwanja wa michezo.

Sehemu ya 5: Vitendo vya kuimarisha ustawi wa kiroho