Nyenzo-rejea 1: Jumuiya ni nini?
Usuli/welewa wa somo kwa mwalimu
Jumuiya ni kikundi cha watu ambao wanashiriki na kuchangia vitu fulani ambavyo vinafanana. Wanajumuiya wanaweza kuishi kwenye eneo moja na wanaweza kuwa na maadili na imani za pamoja. Kunaweza pia kuwa na vitu wanavyomiliki kwa pamoja.
Kama unajaribu kuelezea wazo la jumuiya kwa wanafunzi wako, unaweza kwanza kwa kutumia mifano wanayoifahamu. Njia nzuri ya kuanzia ni kuwaambia waeleze kuhusu familia zao, ikiwepo familia pana ya shangazi, wajomba na binamu. Wasaidie wang’amue kuwa familia zao zinaundwa na mtu mmoja mmoja, mkusanyiko wa watu, wanaoishi sehemu fulani – jumuiya ndogo.
Ili kuimarisha mawazo haya, unaweza kuwaambia kuongeza makundi mengine wanayoshirikiana nayo ambayo wanaunda sehemu ya jumuiya pana zaidi:
Majirani zao, wanaoishi kwenye mtaa mmoja;
Rafiki zao, wanaowaona kila situ.
Rafiki za wazazi wao, ambao wanawatembelea.
Ni mkusanyiko huu wa makundi mbalimbali ya watu ambao unaunda jumuiya, na ni jinsi wanafunzi wanavyoshirikiana na makundi haya kunakochangia jinsi walivyo na jinsi wanavyojiona wenyewe ndani ya jumuiya. Kubainisha mambo mbalimbali yanayosaidia kuelezea jumuiya kutawasaidia kwelewa nafasi waliyonayo katika makundi mbalimbali. Ungeweza kuwaambia waeleze:
eneo – mahali watu wanapoishi; lugha – jinsi watu wanavyoongea; utamaduni – watu wanavaa nguo gani, chakula wanachokula, dini zao; historia – matukio muhimu ambayo yametokea kwa kundi la watu
Somo la 3