Nyenzo-rejea ya 4: Igizo kuhusu mahusiano ya kijumuiya
Nyenzo-rejea ya Mwalimu ya kutumia katika kupanga au kurekebisha pamoja na wanafunzi
Hapa pana baadhi ya maoni kwa ajili ya maigizo-kifani ambayo unaweza kuyafanya pamoja na wanafunzi wako. Ni Maoni tu ya kukufanya uweze kuanza somo. Je, unaweza kufikiria mazingira muafaka kwa ajili ya jumuiya na wanafunzi wako mwenyewe? Kama ndiyo, andika maigizo- kifani yako mwenyewe au rekebisha haya hapa chini. Unaweza kukatisha kila hadithi sehemu tuliyoachia na kuwaambia wanafunzi wamalizie wenyewe. Kwa njia hii, wanafunzi wanaweza kufanya kazi kwenye vikundi na kuja na masuluhisho ya matatizo mbalimbali. Au unaweza kumalizia kwa kuandika mwisho wako mwenyewe wa hadithi hiyo ili kueleza pointi unayotaka.
Godfrey akutana na Chifu
Godfrey alikuwa na tatizo na jirani yake ambaye alikuwa akiendelea kuwaruhusu mbuzi wake kwenye bustani ya Godfrey ambako waliweza kula mboga zake zote za majani. Ilikuwa imeshatokea mara nyingi. Godfrey alijaribu kuzungumza na jirani yake lakini hakumsikiliza. Mwanzoni jirani yake alikuwa mpole, lakini baadaye akawa mara nyingi kwenye sehemu za bia bila kujali sana kuhusu nyumba yake au rafiki zake.Godfrey aliamua kwenda kwa chifu kuomba ushauri.
Bwana Elias muuza duka
Bwana Elias ana duka dogo ambalo huuza chakula na vyombo vya nyumbani. Duka lake ni msaada mkubwa kwa wanawake kijijini kwani linawaokoa kutembea hadi kwenye mji mwingine. Bwana Elias anasifikika kwa kumiliki friji na jenereta. Sasa anaweza pia kuuza vitu baridi kama, vinywaji baridi na maziwa – hata nyama. Vijana wanapenda kwenda dukani kwake kununua kola. Siku moja, Bwana Elias alipokuwa amekazania kumhudumia kijana mmoja kumuuzia pipi, vijana wengine wawili walifungua friji yake na kuiba chupa mbili za kola. Aliudhika sana na aliamua.
Yahsin na babu yake
Babu yake Yahsin ni mzee sana. Ana miaka 92! Anaishi na Yahsin na dada zake watatu na mama yake pamoja na shangazi na mtoto wa huyo shangazi. Muda mwingi babu hukaa chumbani kwake au kwenye kivi chake maalum nje ya mlango wa mbele chini ya kivuli cha mwembe. Mara nyingi anahamaki na kulalamika kuhusu kelele wanazopiga watoto. Mama yake Yahsin humwambia Yahsin kuwa hawana budi kumtunza babu kwani ni mkuu wa nyumba yao. Babu hupata malipo yake ya uzeeni kutoka serikalini, ambayo yanasaidia kununulia chakula chao. Yahsin anamwogopa sana babu yake na anapendelea kuwaachia dada zake ili wamtunze.
Siku moja, dada zake wote wanakwenda kuteka maji na mama anamwambia Yahsin kuwa ni lazima ampelekee babu yake mlo wake wa jioni. Yahsin anaogopa sana. Anachukua chakula na kisha
Nyenzo-rejea ya 3: Sheria/Kanuni za familia moja