Nyenzo-rejea ya 6: Mgogoro katika jumuiya
Nyenzo-rejea ya Mwalimu ya kutumia katika kupanga au kurekebisha pamoja na wanafunzi
Ilitokea vita kubwa baina ya makundi matatu ya kitamaduni ya Mpanga, jumuiya ya kijiji iliyoko kando kando ya barabara kuu. Ilisababisha mauaji ya wanajumuiya kutoka makundi mbalimbali ya kitamaduni na iliathiri jumuiya vibaya sana.
Makundi haya matatu yalikuwa ni Wakwavi, ambao walikuwa wachunga ng’ombe; Wakete, ambao walikuwa wafanya biashara na anga, ambao waliendesha teksi na usafiri. Vita vilianza baina ya Wakete na Wapanga na kutokea hapa vilisambaa.
Wakete walisema kuwa Wapanga walikuwa wanawatoza fedha nyingi sana za kuwasafirishia bidhaa, na watu Wapanga walisema kuwa Wakete walitoza kiasi kikubwa kwa ajili ya mafuta ya kuendeshea teksi zao.
Kwanza kulikuwa na mgomo wa teksi, na baadaye walisitisha kuwauzia vita. Siku moja, kulikuwa na mapigano kati ya dereva wa teksi na mfanyabiashara sokoni. Kisha madereva wote wa teksi walikwenda sokoni kuvunja mabanda yao, na mapigano makubwa yalianza.
Baada ya hili, Wapanga na Wakete walianza kushambulia makazi ya kila mmoja. Waliumizana vibaya. Watu walikufa na mali ilipotea. Familia za makundi haya mawili ziliyakimbia makazi yao kwa ajili ya kutafuta usalama.
Mwanzoni, wachunga ng’ombe wa Kwavi hawakuathirika sana kwa sababu walikuwa kwenye makazi yao na walikuwa wengi. Lakini mapigano yaliendelea kwa siku nyingine na walihusishwa.
Habari hizi za kusikitisha zilifika mapema katika maeneo ya makazi ya watu wa Panga na Kete kuhusu matatizo katika maeneo ya Kwavi. Wakazi waliwashambulia Wakwavi katika jumuiya zao wenyewe, huku wakiwaua ng’ombe. Baadhi ya sehemu, wachunga ng’ombe waliuawa pia.
Hakukuwa na amani kwa siku kadhaa. Nyama haikupatikana majumbani kwa watu Wapanga na Wakete kwa sababu Wakwavi walikuwa wameondoka. Ariya kulikuwa hakuna teksi mitaani. Soko lilikuwa tupu kwa sababu vibanda vilivunjwa na hakukuwa na chakula kingine wala nyama iliyoweza kununuliwa kupelekwa nyumbani.
Viongozi wa jumuiya mbalimbali za Mpanga waliitisha mikutano na kuhutubia makundi yote matatu ya kitamaduni. Walionesha watu jinsi kila mtu alivyohitajiwa na mtu mwingine katika kujenga na kuendeleza jumuiya vizuri. Walieleza jinsi ilivyo muhimu kujifunza kusikiliza maoni ya kila mmoja, na kuwa wavumilivu kwa kila mmoja, kwa sababu kila mtu ana mambo mengi ya kujipatia toka kwa mtu mwingine.
Kisha walikaa na wawakilishi wa jumuiya mbalimbali na kujua chanzo cha tatizo. Walipata suluhisho na walileta amani miongoni mwa watu.
Nyenzo-rejea ya 5: Jumuiya zinazoingiliana kitamaduni