Nyenzo-rejea 2: Kuwatumia viranja wa darasa
Taarifa za msingi / welewa wa somo wa mwalimu
Ukiwa mwalimu, unaweza kuwatumia wanafunzi ili wakusaidie katika shughuli za kila siku za usimamizi wa darasa lako. Kuna majukumu kadhaa rahisi ambayo unaweza kuwaambia wanafunzi wako wayatekeleze kwa niaba yako, nah ii inaleta faida mbili:
Inakuruhusu utumie muda zaidi katika kuandaa na kufanya ufundishaji mzuri, kuliko kutumia muda huo kulisimamia na kulipanga darasa;
Inawapa wanafunzi maeneo machache ya uwajibikaji, jambo ambalo linawatia moyo wa kuonea fahari masomo yao.
Kuna mambo machache unayohitaji kuyafikiria unapochagua viranja wa darasa. Unataka wanafunzi ambao watatekeleza majukumu yao vizuri, na ambao watakuwa tayari kukusaidia wewe na wengine.
Vilevile, unataka wanafunzi ambao watakuwa na jukumu la kuwasiliana vizuri na wengine. Wakati mwingine, wanafunzi wanaweza kuona kwamba kuwa kiranja wa darasa ni kama kuwa na nafasi ya nguvu dhidi ya wengine, na wanaweza kuitumia vibaya dhana hiyo. Ni muhimu kuwasaidia ili waelewe kwamba wanapaswa kutekeleza majukumu yao kwa uaminifu, na wewe hapa utakuwa mfano wa kuigwa. Wanafunzi wote lazima wapewe fursa ya majukumu haya ya ukiranja wa darasa. Ikiwa utawachagua wanafunzi wale wale kila mara, wengine watajihisi kutothaminiwa. Unatakiwa kutoa mwongozo na msaada kwa viranja wa darasa. Baadhi yao watahitaji msaada zaidi yaw engine katika hatua za awali.
Unahitaji kufikiri kwa makini kuhusu kila kazi kabla ya kuzitoa kwa wanafunzi. Kama si kazi ya kufanya kila siku, wanafunzi watachoshwa nayo na wataipuuza. Vilevile, inahitajika kuwepo na kusudi dhahiri kwa ajili ya kazi hiyo, kuliko kitu cha kupitisha wakati tu. Mwisho, utahitajika pia kutoa maelekezo thabiti.
Ni muhimu kugawa kazi na kumpa kila mwanafunzi zamu. Kama wanafunzi wengine hawashirikishwi, watakata tama na wanaweza hata kuvuruga utaratibu wa darasa ili wavute usikivu wa viranja wa darasa; yaani wawasumbue.
Kama ikiwezekana, waache wanafunzi wachague kazi wanazoweza kuzifanya ili kusaidia. Unaweza pia kufanya mikutano ya darasa ya mara kwa mara ambako wanafunzi wanaweza kutoa mapendekezo mbalimbali ya majukumu.
Mwisho, unahitaji pia kuwafuatilia na kuwasaidia. Wasifu pale unapoweza kufanya hivyo na wape mwongozo panapohitajika.
Nyenzo-rejea 1: Faida za sheria za darasa