Nyenzo-rejea 3: Dhima ya walimu
Usuli / dokezo kwa mwalimu
Walimu wana nafasi ya kutambua pindi wanafunzi wanaponyanyaswa. Wana nafasi ya kumfahamu vizuri mwanafunzi mmoja mmoja, na hivyo kung’amua mabadiliko katika tabia au utendaji wa mtoto, ambao unaweza kuhusishwa na unyanyaswaji. Watoto pia wanaweza kufichua hali zao katika masomo ya stadi za maisha au sehemu nyingine za mtaala.
Kama mwalimu atashuku unyanyasaji, njia inayofaa kufuata ni hii:
Anza kukusanya taarifa pindi tu ushukupo unyanyasaji wa mtoto.
Endelea kufanya hivyo kwa uthabiti, andika taarifa zote unazokusanya.
Zichukulie taarifa hizi zote kuwa ni siri.
Jadili tuhuma zako na taarifa ulizokusanya na mwalimu mkuu (kama hahusiki)
Hakikisha usiri kwa kufungua jalada la pekee kwa mwanafunzi huyo. Jalada hilo lapaswa kuhifadhiwa mahali pa salama.
Mwalimu mkuu na mwalimu lazima wachunguze orodha ya vigezo vya utambuzi wa aina mbalimbali za unyanyasaji kuthibitisha taarifa hiyo kabla ya kutoa madai ya unyanyasaji wa mtoto. Washirikishe wataalamu wenye uzoevu.
Usipendelee upande wowote wakati wote na usiruhusu mambo binafsi au hisia au mawazo uliyokuwa nayo kabla yaharibu uamzi wako.
Taarifa yoyote ihusuyo unyanyaswaji wa mtoto ni ya siri na lazima ishughulikiwe kwa busara.
Utoaji taarifa na uchunguzi wa unyanyaswaji wa mtoto lazima vifanyike kwa namna itakayohakikisha usalama wa mtoto.
Haki isihatarishwe, kanini wakati huo huo msaada ambao mtoto na familia yake wanahitaji usipuuzwe.
Mambo mengine muhimu ya kukumbuka unapoongea na wanafunzi ni:
Usimwambie mtoto anayefichua unyanyasaji kwamba humwamini.
Shadidia ujasiri wa mtoto kwa kufanya ufichuzi.
Mwambie mtoto unachotaka kufanya kuhusu aliyokwambia, na kwa nini.
Kama inawezekana, mwambie mtoto kitakachofuata.
Ikilazimika, mtoto apate ushauri-nasaha.
Jiandae kutoa ushaidi mahakamani kama kuna mashataka.
Kuna mashirika mengi Afrika yote yaliyojitoa kwa ajili ya uzuiaji wa unyanyasaji wa watoto, kwa mfano Mtandao wa Afrika kwa ajili ya Uzuiaji na Ulinzi dhidi ya Unyanyasaji na Upuuzaji wa Watoto (African Network for the Prevention and Protection against Child Abuse and Neglect (ANPPCAN)). Tazama Wavuti www.anppcan.org/ [Kidokezo: shikilia Ctrl na ubofye ili uifungue katika kichupo kipya (Ficha kidokezo)] kwa ajili ta taarifa zaidi.
Mkombozi ni shirika lililoanzishwa kwa lengo la kuwasaidia watoto wa mitaani; sasa ni mojawapo ya mashirika maarufu yanayomlenga mtoto kaskazini mwa Tanzania. Nia yao ni ‘kutumia elimu, utafiti, utetezi, na elimu-masafa kuwasaidia watoto na vijana wenye uwezekano wa kudhurika kukua kiakili, kimwili na kiroho’. Unaweza kupata taarifa zaidi kuhusu kazi yao kwenye wavuti http://www.mkombozi.org/
Angalizo: Siku ya Unyanyaswaji wa Mtoto Duniani ni 19 Novemba kila mwaka.
Imetoholewa kutoka kwenye Nyenzo-rejea Zinazolenga Uzuiaji wa Unyanyasaji na Upuuzaji wa Watoto (Resources Aimed at the Prevention of Child Abuse and Neglect) (RAPCAN)
Nyenzo-rejea 2: Aina za unyanyasaji