Nyenzo-rejea ya 2: Jinsia – unafikiri nini?
Matumizi ya mwanafunzi
Soma kila fungu la maelezo kisha chora kiduara kuzunguka tarakimu uliyochagua kuonesha ni kiasi gani unakubaliana au hukubaliani na maelezo.
5 inamaanisha unakubaliana kabisa.
1 inamaanisha hukubaliani kabisa.
Ikiwa huelewi chochote, unaweza kuzungushia 3.
a | Wavulana wana nguvu zaidi kuliko wasichana | 1 | 2 | 3 | 4 | 5 |
b | Kupika ni kazi ya wasichana | 1 | 2 | 3 | 4 | 5 |
c | Wasichana hawana muda wa kujisomea kwa sababu ya kazi zao za nyumbani | 1 | 2 | 3 | 4 | 5 |
d | Wasichana huamka kabla ya wavulana | 1 | 2 | 3 | 4 | 5 |
e | Shuleni, wasichana hufanya kazi nyingi kuliko wavulana | 1 | 2 | 3 | 4 | 5 |
f | Wavulana wana akili zaidi kuliko wasichana | 1 | 2 | 3 | 4 | 5 |
g | Elimu ni muhimu zaidi kwa wavulana kwa vile ni lazima wahudumie familia zao watakapokuwa wakubwa | 1 | 2 | 3 | 4 | 5 |
Nyenzo-rejea ya 1: Masuala ya kijinsia