Sehemu ya 4: Kutalii mazingira
Swali Lengwa muhimu: Utapataje takwimu ili kuendeleza ujifunzaji wa wanafunzi kuhusu mazingira
Maneno muhimu: mazingira, kukusanya data, tathmini, shajara, hadithi za maisha halisi.
Matokeo ya ujifunzaji
Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:
Kutumia hadithi halisi, umekusanya data na umeandika shajara ili kuendeleza welewa wa masuala ya mazingira;
Kupanga, kutekeleza na kutafakari utendaji kuhusu masuala ya mazingira;
Kutathmini ujifunzaji wa darasa na mafanikio ya mradi.
Utangulizi
Suala muhimu duniani ni athari za watu kuhusu mazingira. Tukit umia vibaya rasilimali na kuchafua mazingira kutakuwa na athari hasi kwa wanyama na mimea, na hivyo tutaifanya dunia iwe hatari kwa vizazi vijavyo.
Ukiwa mwalimu, na raia mwema, unahitaji kuelewa masuala ya mazingira na kuchukua hatua kama mfano kwa wanafunzi wako na kuwasaidia kuelewa masuala haya. Unaweza kufanya hivyo kwa kuwapa shughuli ambazo zinahusisha ukusanyaji wa taarifa kuhusu mazingira, katika sehemu zao au katika sehemu pana zaidi, na kutumia taarifa hizo kufikiria kuhusu matokeo ya matendo mbalimbali.
Nyenzo-rejea ya 2: Karatasi-kazi kwa ajili ya ziara sokoni