Nyenzo-rejea ya 1: Matatizo ya upatikanaji wa maji
Mfano wa kazi ya wanafunzi/Nyenzo-rejea ya Mwalimu ya kutumia katika kupanga au kurekebisha pamoja na wanafunzi
Umbali wa kusafiri/kutembea ili kupata maji.
Kuwaacha watoto wadogo nyumbani na kwenda kutafuta maji.
Wanafunzi kutokwenda shule kwa ajili ya kwenda kuchota maji.
Je, maji ni safi na salama?
Ujazo wa vyombo vya kuchotea maji na uzito wa kubeba kwa masafa marefu.
Muda unaotumika kutafuta maji unawazuia watu kufanya mambo mengine.
Maji yanayochotwa yanaweza kuwa yamechanganyika na uchafu na kutumiwa na wanyama.
Hatari ya maambukizi ya magonjwa yanayosababishwa na utumiaji wa maji machafu.
Ukame unaweza kukwamisha upatikanaji wa maji safi.
Ukosefu wa miundombinu k.v. mabomba na vyombo vya kuhifadhia maji yatokanayo na mvua, n.k.
Ukosefu wa mifumo ya kusafisha maji.
Ukosefu wa elimu kuhusu njia za kutumia na kutunza rasilimali asilia za maji/vyanzo vya maji.
Hakuna upatikanaji endelevu wa maji.
Somo la 3