Nyenzo-rejea ya 2: Hali ya darasa
Usuli/welewa wa somo kwa mwalimu
Wanafunzi wanaweza kuyapokea masomo ya VVU na UKIMWI kwa njia tofauti. Wanaweza :
kuuliza maswali ili kujaribu kukuudhi;
kukaa kimya kwa sababu ya maudhi yao wenyewe;
kujaribu kushtuka au kushangaa kutokana kwa kueleza tabia ya ngono waziwazi;
Kukuliza maswali binafsi kuhusu maisha yako mwenyewe;
Kutoa hoja ambazo zenyewe zitaleta mzaha/bezo au ukosoaji kwa wanafunzi wengine.
Ili kukabiliana na hali hizi, ni muhimu uweke kanuni za darasa. Kanuni hizo lazima ziwe wazi kwa wanafunzi kabla ya kuanza darasa. Unaweza kuwaacha wanafunzi wajadiliane na kuweka kanuni zao wenyewe au unaweza kuanza na orodha ya kanuni na kuijadili kama ziko sahihi na kueleza sababu za kanuni hizo kuwa muhimu. Orodha yako inaweza kujumuisha kanuni kama vile:
Wanafunzi wanatazamiwa kuchukuliana vizuri na kujali hisia za kila mmoja.
Wanafunzi hawatakiwi kujadili mambo binafsi ya wenzao yaliyosemwa darasani na watu walioko nje ya darasa.
Wanafunzi lazima waepuke kuingilia kati mazungumzo ya wenzao.
Wanafunzi lazima wasikilizane na kuheshimu maoni ya wengine.
Wanafunzi na walimu wana uwezo wa kuendelea bila kuhoji au kujibu iwapo maswali yanamhusu mtu binafsi.
Hakuna kukatishana tama-hata kama hukubaliani na mtu kwa kiasi chochote, usicheke, usifanye utani dhidi yake au kutumia lugha ambayo itamfanya huyu mtu ajione mnyonge.
Wanafunzi watapewa fursa ya kutoa maswali yao kwa njia ya siri bila kujulikana kwa mwalimu.
Kumbuka kwamba kanuni hizi ni kwa ajili ya walimu na wanafunzi pia!
Mbinu zinazoweza katika ufanisi wa masomo
Mara nyingi vijana wanachekacheka kama mada inayohusu ngono. Hali hii ni lazima iruhusiwe mwanzoni kwani itapunguza vizuizi wakati wa kujadiliana suala la kujamiiana lakini itawasaidia ili wawe wasikivu.
Shughulikia kauli ambazo zinapinga au kudumisha mtazamo pogofu kuhusu waathirika waVVU (mf. kauli zinazoashiria kuwa baadhi ya makundi ya kikabila yanahusika na mlipuko wa UKIMWI) kwa kujadili madhara ya kauli kama hizi.
Kuwa na mamlaka unaposhughulikia hali ngumu – mf. Mada hiyo si sahihi/haiendani na darasa hili. Kama ungependa kuijadili, nitafurahi kuzungumza na wewe baada ya darasa.
Epuka kuwa mkali kuhusiana na majibu yanayotolewa ili wanafunzi wapate moyo wa kueleza maoni yao kwa uwazi na kwa uaminifu.
Elezea pande zote mbili za suala linalotatanisha.
Epuka kutoa hukumu kuhusu kile kilichosemwa.
Kuwatenganisha wavulana na wasichana wakati wa kufanya kazi kwa vikundi kunaweza kusaidia pale mjadala unapoweza kusababisha maudhi, au pale ambapo kwa kuwatenganisha huku hivi vikundi vitafanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Unajua kuwa wajibu wako mkubwa ni kuhakikisha kwamba unafahamu ukweli unapofundisha kuhusu VVU na UKIMWI. Lazima ujiandae kikamilifu na hili litakusaidia ujiamini katika kushughulikia mada hii ngumu.
Inasaidia kufikiria kabla jinsi utakavyopokea taarifa za wanafunzi wanaoamini kuwa wameshaathirika. Ni muhimu kwamba upokee taarifa hizi kwa namna itakayowafanya wanafunzi wenye wasiwasi kujihisi faraja kutaka ushauri wako.
Ni muhimu kwamba umsikilize mwanafunzi yeyote anayekujia, pasipo kumlazimisha afuate maadili au mawazo yako, au kumhukumu. Jaribu usiulize maswali elekezi au dokezi (yanayoelekeza kwenye majibu) kuhusu mienendo yao.
Sehemu ya maandalizi yako yapasa kujumuisha kujua hudumu gani za VVU na UKIMWI zinazopatikana katika jumuiya yako. Tafiti ni kliniki au AZAKI zipi hutoa ushauri na msaada wa VVU na UKIMWI kwa vijana ili ujue wapi pa kuwaelekeza wanafunziwako ikilazimika.
Eleza shauku yako juu ya afya ya mwanafunzi husika, na, ikifaa, mwambie kuwa unafahamu kuhusu huduma zinazoweza kusaidia. Jitolee kuanza mchakato kwa kuwasiliana na kituo ambacho mwanafunzi anachagua.
Endeleza msaada wako kwa kumwuliza mwanafanzi mara kwa mara kama anahitaji taarifa zaidi, kama ameshachukua hatua zozote au bado ana shaka juu ya lolote kuhusiana na maongezi yenu.
Imetoholewa kutoka Elimu ya Afya Shuleni Kuzuia VVU & UKIMWI (1999), Shirika la Afya Duniani/UNESCO (School Health Education to Prevent AIDS & STD (1999) World Health Organisation/UNESCO).
Nyenzo-rejea ya 1: VVU na UKIMWI katika Afrika