Nyenzo-rejea 3: Jaribio kuhusu VVU na UKIMWI

Utumizi wa Mwanafunzi

Jaribio hili lipo mtandaoni kwenye http://www.avert.org/ generalquiz.htm [Tip: hold Ctrl and click a link to open it in a new tab. (Hide tip)] na unaweza kulifanya mwenyewe hapo. Kama wanafunzi wako wanaweza kupata mawasiliano ya Tovuti, unaweza kuitumia nao. Kama haiwezekani, hapa kuna nakala ya matini. Weka tiki kwenye jibu udhanilo ni sahihi.

1. Je, VVU huathiri mashoga na wasagaji tu?
NdiyoHapanaMashoga tuWasagaji tu

2. Ni kadiri ya watu wangapi wanaoishi na VVU dunia nzima?
Milioni 38.6Milioni 25.8Milioni 3.5

3. Utatambuaje kuwa mtu ana VVU au UKIMWI?
Kutokana na jinsi wanavyotendaHuonekana wamechoka na wagonjwaHakuna njia rahisi ya kuwatambua

4. Unaweza kupata UKIMWI kwa kuchangia kikombe na mwathirika?
NdiyoHapanaKama kikombe hakikuoshwa

5. UKIMWI ulifafanuliwa kwa mara ya kwanza lini?
199719871982

6. Ni kitu kipi hukulinda zaidi dhidi ya uambukizo wa VVU?
Kondomu 

Vidonge vya Kuzuia

Uzazi

Jeli ya Kuua Manii

7. Dalili mahususi za UKIMWI ni zipi?
Hakuna dalili mahususiUpele toka kichwani hadi unyayoniUnaanza kuonekana mchovu

8. VVU ni nini?
KirusiBakteriaKuvu

9. Je, wadudu wanaweza kueneza VVU?
Mbu tuNdiyoHapana

10. MKN kirefu chake nini?
 

Maambukizi Kupitia

Ngono

 

Mganga Kabili wa

Ngono

 

Muuguzi Kamili wa

Ngono

11. Je, kuna tiba ya UKIMWI?
NdiyoHapanaZipo kwa agizo la daktari

12. Siku ya UKIMWI Duniani huadhimishwa lini?
1 Januari1 Desemba1 Juni

13. Duniani kote, UKIMWI umeathiri zaidi kundi la umri upi?
Miaka 0–14Miaka 15–24Miaka 25–34

14. Kuna tofauti baina ya VVU na UKIMWI?
Ndiyo, VVU ni kirusi kisababishacho UKIMWIHapana, VVU na UKIMWI ni kitu kile kileNdiyo, UKIMWI ni kirusi kisababishacho VVU

15. Ni asilimia ngapi ya wale walioambukizwa VVU ni wanawake?
Karibu 25%Karibu 50%Karibu 75%

16. Inawezekana kupunguza hatari ya mwanamke aliyeambukizwa VVU kukiambukiza kichanga chake?
Ndiyo, hatari inaweza kupunguzwa ikawa chini zaidiHapana, haiwezekaniKiasi tu

Majibu

Swali 1.

Jibu – Hapana

Swali 2.

Jibu – Milioni 38.6

Swali 3.

Jibu – Hakuna njia rahisi ya kutambua

Swali 4.

Jibu – Hapana

Swali 5.

Jibu – 1982

Swali 6.

Jibu – Kondomu

Swali 7.

Jibu– Hakuna dalili mahususi

Swali 8.

Jibu – Kirusi

Swali 9.

Jibu – Hapana

Swali 10.

Jibu – Maambukizi Kupitia Ngono

Swali 11.

Jibu – Hapana

Swali 12.

Jibu – 1 Desemba

Swali 13.

Jibu – Miaka 15–24

Swali 14.

Jibu – Ndiyo, VVU ni kirusi kisababishacho UKIMWI

Swali 15.

Jibu – Karibu 50%

Swali 16.

Jibu – Ndiyo, hatari inaweza kupunguzwa ikawa chini zaidi

Nyenzo-rejea ya 2: Hali ya darasa

Nyenzo-rejea 4: Uambukizo