Nyenzo-rejea 4: Uambukizo
Nyenzo-rejea ya mwalimu kwa ajili ya kupanga au kubadilisha kwa ajili ya kutumia na wanafunzi/Matumizi ya wanafunzi
Unaweza kutumia mbinu hii kwa kundi lolote la rika kwa kubadili maswali yawiane na kiwango cha watoto. Maelezo haya yanawafaa zaidi wanafunzi wakubwa zaidi wa shule za msingi.
Madhumuni
Kutathmini viwango vya utambuzi wa jinsi VVU vinavyoenezwa.
Kuhimiza wana-vikundi kufikiria njia mbalimbali za uambukizo.
Vitu utakavyohitaji
Chumba chenye nafasi ya kutosha, ili kuruhusu upitaji huru wa hewa. Au unaweza kuwa nje.
Nakala ya karatasi ya maswali ya kweli/si kweli kuhusu Uambukizo na karatasi ya Majibu.
Karatasi mbili kubwa zenye maandishi ya wazi ‘NAKUBALI KABISA’ na ‘SIKUBALI KAMWE’.
Pini.
Muda – usiopungua dakika 60 kutegemea idadi ya kauli zilizotumiwa na ukubwa wa kundi.
Unafanya nini
Weka karatasi zenye maandishi 'NAKUBALI KABISA' na 'SIKUBALI KAMWE' kwenye kuta zinazokabiliana au kwenye kuta/miti uwanjani.
Waeleze wana-kundi kwamba utasoma mfuatano wa kauli, mojamoja. Kila mtu afikirie kama anakubaliana nayo au hakubaliani nayo, kisha aende upande wa chumba au nafasi iliyo na jibu husika. Ni sawa tu kukaa katikati kama hawana hakika.
Soma kauli ya kwanza. Baada ya watu wote kujongelea mahali/nafasi waliyochagua, watake wachague mtu aliye karibu wajadiliane nao kwa nini wamesimama hapo.
Sasa watake watu wachague mtu aliye mbali nao wajadiliane nao kauli, kila mmoja akieleza kwa nini amechagua kuwa hapo alipo.
Fanya hivyo kwa kauli nyingi iwezekanavyo kulingana na muda uliopo.
Kutana tena kama kundi, na, huku ukizungukazunguka, mtake kile mtu ataje jambo ambalo linamkanganya au ambalo halielewi vizuri. Watake wanakundi wafafanue masuala husika na usaidie tu pale inapolazimu.
Matokeo yanayowezekana
Mwishoni mwa zoezi hili, itakuwa wazi kuwa sehemu zenye mashaka zitabaki. Watu mmoja mmoja watakuwa wamepata nafasi ya kufikiria juu ya njia za kuambukiza VVU, na kujadili njia hizi na wanakikundi wengine. Itakuwa wazi pia kwamba njia za uambukizaji wa VVU ni mahususi sana, k.m. si ngono inayoambukiza virusi bali ngono isiyo salama inayohusisha mpenyo. Watu wanaweza mara nyingine kuwa wagomvi wakati wa kufanya zoezi hili, hivyo unahitaji kuingilia kati kuamua ugomvi.
Kweli | Si kweli | ||
1. | Unaweza kuambukizwa VVU kwa kuwa mwasherati | ||
2. | Udungaji wa madawa ya kulevya kutakwambukiza VVU | ||
3. | Unaweza kupata VVU kwenye kikalio cha chooni | ||
4. | Kama u mzima huwezi kuambukizwa VVU | ||
5. | Wana-ndoa hawaambukizwi VVU | ||
6. | Kama utakuwa na mwenzi mmoja huwezi kuambukizwa VVU | ||
7. | Kama wanawake watatumia kingamimba hawawezi kuambukizwa VVU | ||
8. | Unaweza kuambukizwa VVU kwa kuchangia miswaki | ||
9. | Kama utafanya ngono na watu waonekanao wenye afya, hutaambukizwa VVU | ||
10. | Kama utafanya ngono na watu uwafahamuo tu, hutaambukizwa VVU | ||
11. | Ngono ya mkunduni baina ya wanaume wawili ni hatari zaidi kuliko ngono hiyo baina ya mwanaume na mwanamke | ||
12. | Unaweza kuambukizwa VVU kutokana na kubusu | ||
13. | Mwanamme anaweza kuambukizwa VVU kama atamfanyia ngono ya kinywa mwanamke | ||
14. | Mwanamme anaweza kuambukizwa VVU kwa kufanyiwa ngono ya kinywa na mwanamke | ||
15. | Kondomu zinaweza kukomesha usiambukizwe VVU |
Karatasi ya majibu ya Kweli/Si kweli
1. Tabia ya uasherati si hatari kama tabia, lakini kufanya ngono isiyo salama na mtu aliyeambukizwa ni hatari. Kwa kutumia kondomu kama inavyopasa na kuepuka ngono ya mpenyo, unaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa hatari ya uambukizo.
- Kama tu sindano au sirinji imechafuliwa kwa VVU kabla.
- Hakuna uambukizo wa VVU unaofahamika kutokana na kukalia vikalio vya vyoo.
- Uwe mwenye afya au uwe na matatizo ya kiafya, kama ukishiriki ngono isiyo salama kuna uwezekano wa kuambukizwa.
- Hii inategemea washirika wahusika, waliyotenda kabla ya kukutana, kama mmojawao alishiriki ngono isiyo salama nje ya ndoa, au kama walijidunga madawa kwa kutumia zana zilizoambukiwa.
- Kama kwa Na 5.
- Ni kondomu tu zinazotoa ulinzi dhidi ya uambukizo wa VVU; na hata kondomu si salama kikamilifu. Njia nyingine za kinga ya mamba hazitoi ulinzi wowote dhidi ya VVU.
- Hakuna ushahidi wa uambukizo kwa njia hii, lakini ni vema kutochangia miswaki kwa sababu za kiafya kijumula.
- Watu wengi wenye VVU huonekana wenye afya kabisa. Hivyo, mwonekano ni njia isiyofaa ya kutathmini hatari.
- Kumfahamu mtu vizuri si jambo lakutegemea katika kufahamu kama mtu ameambukizwa VVU au la.
- Ngono ya kinywani ni hatari pia ifanyike baina ya wanaume wawili au baina ya mwanaume na mwanamke.
- Hakuna ushahidi wa uambukizo wa VVU kwa njia hii, ingawa kubusiana wakati kukiwa na vidonda mdomoni kunaweza kuwa hatari.
- VVU viko kwenye ute wa mlango wa kizazi na uke kadhalika na damu ya hedhi, hivyo upo uwezekano wa kuambukizwa kwa njia hii.
- VVU viko katika shahawa, hivyo kuna uwezekano wa uambukizo kwa njia hii.
- Kondomu zikitumika ipasavyo husaidia kuzuia uambukizo wa VVU kutoka kwa mshirika aliyeambukizwa kwenda kwa mshirika ambaye hajaambukizwa. Hata hivyo, kondomu si salama asilimia 100%. Vilainisho vikitumika vyapasa viwe vya majimaji kwani kama ni vya mafuta vitadhoofisha kondomu. Wakati wa kununua kondomu kagua tarehe ambapo kondomu hiyo inapaswa kuwa imeuzwa.
Nyenzo-rejea 3: Jaribio kuhusu VVU na UKIMWI