Somo la 1

Kwa kuanzia, unahitaji kukusanya vitu mbalimbali ambavyo unaweza kuvitumia kwa ajili ya shughuli za sehemu hii (Angalia Nyenzo-rejea 1: Kutumia mifuko laini ). Inaweza kusaidia kukusanya na kuwa na sanduku la vitu hivyo kwa ajili ya matumizi ya baadaye ya kudumu. Wanafunzi wanaweza kufurahia kukusaidia kukusanya vitu hivyo, na ‘kuangalia maumbo mbalimbali’ katika maisha ya kila siku. (Kumbuka kuwasifu wanafunzi wako watakaochangia vitu hivyo, na kuchukua nafasi hiyo kujadili umbo la kitu chochote waletacho.)

Uchunguzi kifani ya 1

Baadhi ya walimu wa hesabu wa shule za msingi Umtata, Afrika ya kusini, walikuwa wanatayarisha utaratibu wa ufundishaji wa somo la jiometri kwa muhula. Kama njia ya maendeleo ya mafunzo kazini, walitaka kutayarisha vyema shughuli za somo la jiometri kwa ajili ya wanafunzi wao. Waliamua kumkaribisha mtaalamu wa hesabu kutoka katika taasisi ya elimu ya juu ili kuwasaidia kuandika mapango wa kazi. Alikubali, na akashauri waanze na shughuli ya uchambuaji. Walihitaji kukusanya vitu vingi kadiri iwezekanavyo, kama vile, makopo yasiyo na kitu, kibonge vya uzi wa pamba, vibingirisho vya karatasi zitumikazo chooni na picha za maumbo mbalimbali kutoka katika mazingira k.m. majengo, sampuli za vitambaa na kadhalika. Wakiwa katika makundi ya watu wawili wawili, walipanga kila shughuli kwa kutumia maumbo haya kwa kujaribu wakiwa peke yao.

Walipokwenda madarasani kwao, walimu waliwataka wanafunzi wao kuwasaidia kukusanya vitu kama vile. Walipopata vitu vya kutosha kwa ajili ya wanafunzi kufanyia kazi katika vikundi vya wanafunzi watano au sita walijaribu shughuli hiyo, kila kikundi kikiwa na vitu tofauti kumi au zaidi vya kuchambua. Kazi zilihusu uwekaji vitu katika vikundi ambavyo vilikuwa na sifa zinazofanana, kurekodi tabia vinavyochangia, na kuonesha ni kitu kipi kilikuwa na sifa hiyo. Walimu walishangaa na kutiwa moyo kutokana na shauku na tafakuri zilitokana na shughuli hiyo miongoni mwa wanafunzi. Katika mkutano wao uliofuata wa mafunzo kazini, kila mwalimu aliripoti kilichotokea.

Shughuli ya 1: Kuwasaidia wanafunzi kutenganisha vitu halisi

Kusanya vitu vingi vyenye maumbo mbalimbali kadri uwezavyo. Utahitaji angalau vitu viwili kwa kila mwanafunzi. Vilevile, unaweza kutumia picha kutoka katika mazingira.

Gawa darasa katika makundi ya wanafunzi watano watano au sita sita na lipe kila kundi fungu la vitu (angalia Nyenzo-rejea 1 ).

Eleza ‘seti’ ni nini –mkusanyiko wa vitu vyenye sifa zinazofanana, kwa mfano, darasa ni ‘seti’ ya wanafunzi, ambao wanafundishwa na wewe. ‘Seti hii kubwa’ inaweza kupangwa katika seti ndogo ndogo –mfano mmojawapo ungeweza kuwa seti ya wavulana, na seti ya wasichana. (Unaweza kufanya utengaji halisi wa wanafunzi katika seti hizi mbili kwa lengo la kufafanua hoja hii.)

Yaeleze makundi kwamba yana seti ya vitu mbalimbali. Watake wachambue vitu hivi katika seti ndogo ndogo. Waulize maswali yafuatayo: Kuna njia ngapi tofauti ambazo unaweza kuzitumia katika kuchambua vitu hivi na kuunda seti? Kufanya hivi kutaifanya shughuli hii iwe huru, kwa hiyo usitaje idadi ya seti zitakiwazo au kigezo chochote.

Waambie waeleze sababu za uchambuaji wao wa kila seti. Wanavyoendelea na kazi, wachunguze na kusikiliza majadiliano wanayoyaendesha katika makundi yao, na weka rekodi ya kile wanachokisema kwa uangalifu. Kufanya hivyo kutakusaidia kujua nani alikuwa na mawazo kamili na nani bado alikuwa anayapima mawazo yake.

Liambie kila kundi kushirikiana na mengine kwa kuwaeleza njia mbalimbali lilizotumia kuchambulia vitu vyake, na weka rekodi ya mambo muhimu yatakayojitokeza ubaoni.

Unaweza kuamua kutumia vipindi viwili katika shughuli hii.

Sehemu ya 1: Kuchunguza maumbo