Somo la 2

Baada ya kutambulisha dhana ya uchambuaji wa vitu, na kuwaambia wanafunzi waeleze tabia za vitu hivyo kwa lugha ya ‘kawaida’, sasa ni wakati muafaka wa kuunda mbinu ya kihisabati zaidi ya kuelezea baadhi ya sifa za vitu hivyo.

Katika kila eneo la kazi, watu huunda maneno na istilahi maalum za kueleza kile wanachokifanya. Lugha maalum ya kihisabati, wakati mwingine, hujulikana kama kioneshi cha kihisabati - mathematical register. Kuwaingiza wanafunzi katika lugha ya maumbo kunachukua muda na kunahitaji kujengwa katika masomo yako kwa kipindi kirefu. Kadri wanavyoelewa dhana zinazowakilishwa na majina husika, ndio

wakati muafaka wa kuanza kuwafundisha maneno ya kihisabati. Pamoja na kutumia maneno haya katika mazoezi, vilevile, unaweza kuwaambia wanafunzi wako waanze kuunda ‘kamusi ya hisabati’ ili iwasaidie kukumbuka maana za istilahi hizo. Nyenzo-rejea 2: Kamusi ya hisabati inatoa mifano sita ya aina za maneno ambayo wanafunzi wanaweza kutumia katika kueleza maumbo wanayoyashughulikia.

Uchunguzi kifani ya 2: Kutumia istilahi za kihisabati katika kuchambua vitu

Bibi Chizoza aliwaambia wanafunzi wake wachambue mkusanyiko wa vitu vyenye maumbo mbalimbali ambavyo aliwapatia. Baadhi ya wanafunzi waliamua kuvipanga vitu kwenye makundi kulingana na mahali vinapotumika katika mazingira ya nyumbani, kama vile chumbani, jikoni na bafuni. Wanafunzi wengine walifanya kazi ya kuchunguza kama vitu vilikuwa vinafanana. Makundi mengine yaliona vigumu kueleza sifa za vitu vyao, kwa mfano, yalisema kwamba baadhi ya maumbo yalikuwa bapa, lakini waliweza kueleza maumbo mengine kama ‘si bapa’ tu.

Kwa kulisawiri darasa zima limzungukalo, Bibi Chizoza alichunguza baadhi ya vitu hivi tatizi vya ‘si bapa’ na wanafunzi. Kwa kutotumia istilahi za kihisabati kwanza, alinza kubainisha sifa fulani (kama vizingo, kingo na kona) na akawaambia wanafunzi waeleze istilahi hizi kwa maneno yao wenyewe.

Kisha, wanafunzi wachache walipoeleza sifa hizi, na kutafakari kuhusu maneno yote wanayoweza kutumia, Bibi Chizoza alianza kuwafundisha istilahi sahihi za kihisabati, na alikubaliana na darasa jinsi ambavyo wangeeleza istilahi hizo kwa maneno yao wenyewe. Aliwaeleza kwamba walianza kujifunza ‘lugha nzuri ya hisabati’ (angalia Nyenzo-rejea 2 kwa ajili ya baadhi ya istilahi za kutumia).

Bibi Chizoza alitengeneza karatasi kubwa ya ukutani na kuiandika maneno mapya ya kihisabati, na fasili walizokubaliana. Aliwaambia wanafunzi waanze kuandika kamusi zao wenyewe za hisabati nyuma ya madaftari yao ya mazoezi, huku wakichora michoro ili kuonesha maana za maneno haya. Waliendelea kukuza kamusi hii nyakati za vipindi vya hisabati vilivyofuata.

Shughuli ya 2: Kueleza vitu vya kijiometri

Kwa kutumia fungu la vitu ulivyokusanya, waite wanafunzi karibu nawe na waoneshe baadhi ya vitu hivyo.

Waoneshe kitu chenye sura ya bapa, halafu waoneshe kingine chenye sura ya mzingo.

Waambie wanafunzi wachukue vitu vingine vyenye sura za bapa, au za mzingo.

Waambie wanafunzi warudi kwenye makundi yao, na lipe kila kundi fungu la vitu.

Kazi yao ni kuweka kila kitu katika mojawapo kati ya seti nne zifuatazo: vyote vyenye sura bapa; vyote vyenye sura za mzingo; vyenye sura bapa na mzingo; nyingine.

Unaweza kuendeleza shughuli hii kwa kuwatambulisha istilahi za kiwango cha juu ‘kipeo’ na ‘kingo’ na kuzitumia katika kuchambua vitu.

Tengeneza jedwali la matokeo yao kwa ajili ya kulitundika darasani.