Nyenzo-rejea ya 1:  Kutumia mifuko ya kuhisi

Nyenzo ya Mwalimu kwa ajili ya kupanga/kurekebisha na kutumia na wanafunzi

Mifuko au maboksi ya kuhisi, ambayo yanaweza kutengenezwa kwa urahisi na wewe au wanafunzi wako (angalia chini) yanaweza kutumika katika mtaala wote kusaidia kukuza ujuzi wa lugha na wa uchunguzi kwa wanafunzi wako. Katika hisabati, ni njia nzuri kuwasaidia wanafunzi kuchunguza tabia za maumbo na vitu. Katika sayansi, unaweza kuchunguza tishu za vitu. Utumiaji wa mfuko au boksi la kuhisi ni motisha kubwa kwa wanafunzi kutokana na uhusishwaji katika mchezo, haja ya kusikiliza kwa makini na hamu ya kukisia jibu sahihi vinavyowasisimua na kuwavutia wanafunzi.

Maoni kuhusu vitu vya shughuli za maumbo

Unaweza kutumia chaguo la michemiraba (dadu, matofali), miche mstatili (maboksi, vipande vya mbao), miche pembetatu (maumbo yenye ‘V’ ya mbao, maksi ya kibunifu ya chokoleti), matufe (mipira), mapiramidi (ya mbao au ya plastiki), micheduara (vibiringisho vya karatasi za chooni, kalamu, vijiti vya pini zisizo na vichwa), pia (kofia za karamuni, aiskrimu za koni). Unaweza pia kujumuisha kitu kimoja au viwili visivyo vya kawaida au vyenye sehemu nusu isiyo ya kawaida (mawe, maganda, majani) ili kuchochea mjadala. Vyote hivi vinaweza kukusanywa mahali wanamoishi wanafunzi ili kusaidia kuhusianisha hisabati na mazingira ya mahali hapo.

Jinsi ya kutengeneza mfuko wa kuhisi

Kwa shughuli hii unaweza kutumia karatasi ya kutengenezea mfuko ambayo huwezi kuona ndani au unaweza kushona mfuko kutokana na kitambaa cha sentimeta zipatazo 30 kwa 30 kikiwa na uwazi sehumu moja ya mwisho. Sehemu ya juu ya mfuko inahitaji kuweza kufungika na kufunguka ili kutumbukiza vitu na kuruhusu mwanafunzi kuingiza mkono na kukihisi kitu kilichomo lakini kwa kuhakikisha kuwa hakuna hata mmoja anayeona kilichomo ndani ya mfuko. Unaweza kutumia mpira unaotanuka au uzi wa kufungia ili kuifanya sehemu ya juu ifungike.

Jinsi ya kutengeneza boksi la kuhisi

Kadi ya ubao yenye ukubwa wowote wa kati inaweza kutumika kutengenezea boksi la kuhisi. Unatakiwa kukata uwazi wa saizi ya mkono katika sehemu moja ya boksi. Hii ni kwa ajili ya kumwezesha mwanafunzi kuingiza mkono ndani ya boksi na kuinua kitu ambacho atakihisi. Baadhi ya watu hukata matobo mawili ili mwanafunzi atumbukize mikono yote miwili ndani ya boksi na kukihisi kitu husika. Unatakiwa kuweka sehemu zilizo wazi mbali na wanafunzi wengine ili wasione kilichomo ndani ya boksi.

Jinsi ya kucheza mchezo

 

Mantiki ya mchezo ni kuficha vitu tofauti, vinachovutia (ambavyo vinafahamika kwa wanafunzi wako) ndani ya mfuko/boksi la kuhisi. Unaweza kutumia maumbo ya kawaida ya bakuli, sufuria, au hata makopo ya vyakula.

Mwanafunzi anakuja mbele na kuhisi kitu kilichomo ndani ya mfuko/boksi la kuhisi. Hakitoi kitu hicho nje au kukionesha kwa wanafunzi wengine. 

Badala yake, mwanafunzi atafakari kwa makini sana kuhusu njia ya kukieleza kitu hicho, bila kutaja jina lake. Anatumia mlango wa fahamu wa kugusa katika kuorodhesha na kueleza uchunguzi wake. Wakati huo huo, mwanafunzi huyo anatakiwa afikiri kwa makini kisayansi na kihisabati. Anatakiwa kufikiri kuhusu tabia ambazo kitu hicho kimeumbwa nazo. Vilevile, anatakiwa kufikiri kwa makini kuhusu umbo, ukubwa na muundo wa kitu hicho.

Kila mara mwanafunzi anapofanya uchunguzi, mwanafunzi mwingine hapo darasani anapewa nafasi ya kujaribu kufikiri kitu hicho ni nini.  

Wakati mchezo huu ukiendelea, mwalimu anaweza kuigiza kama mwandishi (au katibu) na kurekodi uchunguzi na makisio ubaoni, au kwenye kipande kikubwa cha karatasi. Mwalimu aandike hoja muhimu tu.

Kitendo hiki kiendelee mpaka mpaka mtu mmoja ataje kwa usahihi kabisa kitu hicho ni nini. Kisha, kitu kitolewe nje ya mfuko/boksi na kuoneshwa kwa wanadarasa.

Ni muhimu kwamba muda mfupi utumike kujadili usahihi wa uchunguzi – ujuzi wa lugha ya kihisabati, ubora wa maelezo, ujuzi wa mawasiliano na hadhi ya makisio.

Nyenzo-rejea ya 2: Kamusi ya hisabati