Sehemu ya 2: Njia za utendaji toka katika karatasi hadi utengenezaji wa mchemraba

Swali Lengwa muhimu: Unawezaje kuwasaidia wanafunzi ‘kuona’ na kubadilika kimawazo kuhusu maumbo ya kijiometri?

Maneno muhimu: wavu; jiometri; upigaji taswira kichwani; mbadiliko/mgeuzo;masanduku; kete; uchunguzi

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • Kutalii njia zinazoweza kutumika katika mazingira ya mahali hapo na neti rahisi za kuwasaidia wanafunzi kuelewa mchoro wa Vivimbe-3 (V3);
  • Kutumia utalii na kukokotoa maswali ili kupanua uwezo wa kufikiri wa wanafunzi wako kuhusu neti tofauti za kutengeneza mchemraba;
  • Kutumia kete kuhimiza upigaji taswira wa kichwa na mgeuzo wa wavu wa mchemraba.

Utangulizi

Fikiria kuwa unahitajika kuchora mchoro katika kipande cha karatasi, ambacho kinaweza kukatwa na kukunjwa katika mchemraba. Katika karatasi utachora vipande sita vya mraba ambavyo vitakunjwa kutengeneza vipande sita vya mraba vya mchemraba. Je, unaweza kufikiria mchoro utakaochora katika karatasi kutengeneza mchemraba?

Sio rahisi kufanya hivyo, kwa kuwa zoezi hili la kufikirika linahitaji stadi mbili muhimu za hesabu –kupiga taswira ya kichwani (kuweza ‘kuona’ taswira ya Vivimbe-2 {V2} au V3 vya kihesabu kwa kutumia jicho la akili yako),na ugeuzi wa kiakili kuweza ‘kuchezea’ au kubadili taswira hiyo kwa namna fulani). Sehemu hii inatalii mbinu za utendaji wa kuendeleza stadi hizi kwa wanafunzi wako wakati wanapotengeneza neti.

(Neti ni kiwakilishi cha V2 vyenye umbo la V3 ambavyo vina mistari ya vitone inayowakilisha mikunjo, na mistari halisi inayowakilisha sehemu ya kukata.) Utengenezaji wa kuiga kitu halisi utawasaidia wanafunzi wako kuona taswira akilini kuhusu mageuzi ya kitu hicho katika hali yake halisi na kuhusisha uelewa wao wa maumbo na maisha yao wenyewe .

Nyenzo-rejea ya 2: Kamusi ya hisabati