Somo la 1

Kadri wanafunzi wako wanavyofanya kazi ni muhimu wajihisi kuwa wanafanya uchunguzi, na kwamba wanafumbua tatizo. Ukiwa mwalimu unatakiwa kufuatilia wakati wanafunzi wakishika usukani katika uchunguzi. Mwanzo, ni vigumu kufanya hivyo, lakini kama unaweza kutafuta njia ya kutayarisha darasa lako linalowapa wanafunzi nafasi ya kufikiri, kuzungumza na kugundua, wengi watakushangaza kwa mawazo na uelewa wao. Kwa taarifa zaidi, angalia Nyenzo muhimu: Kutumia ugunduzi darasani.

Shughuli 1 na Uchunguzi kifani 1 vinatalii njia za kuwaruhusu wanafunzi kugundua wenyewe neti kwa ajili ya maumbo tofauti.

Uchunguzi kifani ya 1: Kuchunguza neti kwa ajili ya chuma

Bibi Sawula wa Afrika ya kusini alikuwa anafanya kazi kuhusu maumbo. Kwanza aliwachukua wanafunzi wake katika mazingira ya mahali hapo kuona maumbo tofauti ambayo wangeyakuta.

Siku iliyofuata, alitaka kuanza somo lake kuhusu neti kwa kuwatayarisha wanafunzi wake kugundua wenyewe neti rahisi.

Bibi Sawula aliwataka kufikiri jinsi ambavyo wangetengeneza maandalizi ya baadhi ya maumbo waliokwishayaona katika karatasi. Alisikiliza baadhi ya mawazo haya. 

Kisha, baada ya kuwaeleza wanafunzi wake kuleta bati (alikuja na baadhi ya bati kwa wale ambao wangesahau au ambao wasingeleta), aliwauliza swali hili walijadili katika makundi: Kopo lenu la bati lenu limetengenezwa kwa kipande cha bati lililo tambarare . Fikiria kuwa karatasi yako ni bati linaloweza kutengenezwa kuwa kopo –ni umbo gani litakalokatwa kutoka katika karatasi? Unaweza kulitumia kopo kukusaidia kuchora umbo hilo katika karatasi yako? Nyenzo rejea 1: silinda inaonesha jinsi V2 vinavyoweza kukunjwa kuwa V3.

Aliwapa wanafunzi muda wa kutegua fumbo hili. Bibi Sawula alifurahia kuwaona wanafunzi wake wakifanya kazi na hakuwaingilia mpaka alipoona dalili za kushindwa.

Alifurahia kuona ni wangapi waliweza kutengeneza neti.

Shughuli ya 1: Kutambua neti ya sanduku tupu

Katika shughuli hii kila mwanafunzi alete sanduku tupu. Na wewe ulete baadhi pia.

Kipe kila kikundi gundi ya maji au gundi ya karatasi na karatasi nne za ukubwa wa A4 (saizi ya barua).

Waambie wanafunzi kuwa kwa pamoja wataweza kugundua jinsi ya kutengeneza kisanduku chenye umbo kama la sanduku (mche wa mstatili –angalia chini), kwa kutumia karatasi zenye ukubwa wa A4 (saizi ya barua) na kwa kuchora, kukunja na kugundisha.

Watake wafanye kazi pamoja na wajadili jinsi ya kuifanya kazi hii kabla hawajaanza. Wakisharidhika na wanachokifanya, waambie watumie karatasi moja kujaribu mawazo yao.

Kama baadhi ya vikundi vimeshindwa, wape fununu ya jinsi ya kuanza kwa kuwaeleza kuwa walifumue sanduku kulifanya tambarare.

Zungukia darasa kimya; usaidie tu kama kikundi kimeshindwa au kimeomba msaada.

Watake katika kila kikundi kuonesha kazi zake darasani.

Katika somo lijalo, watake wanafunzi walipambe sanduku lao na walitundike kutoka katika dari.

Mwisho, watake waandike mipango yao au neti kwa ajili ya masanduku waliyotengeneza na waoneshe kazi hizi pia.

Sehemu ya 2: Njia za utendaji toka katika karatasi hadi utengenezaji wa mchemraba