Somo la 2

Baada ya kuwa na uzoefu wa neti, na kuchora maumbo ya mchemraba kutokana na neti hizo, sasa utaendelea kutafuta njia za kuwasaidia wanafunzi wako kupiga taswira na kufanya mageuzi ya neti hizi kiakili. Njia mojawapo ya kufanya hivyo ni kutumia kete. Njia nyingine ni kuangalia maumbo katika mazingira.

Kete ni mchemraba maalum, ambapo kila upande una namba tofauti kati ya namba 1 hadi 6, na namba katika sehemu ya pili hufanya jumla ya 7. Angalia Nyenzo rejea 3: Ukweli kuhusu kete.

Ili kuwekea mraba namba katika mchemraba wa neti, kabla haijakunjwa katika mchemraba, wanafunzi wanapaswa kupiga taswira kwa usahihi mageuzi kutoka sehemu V2 na kuwa sehemu za V3 katika uelewa wa akilini. Uchunguzi kifani 3 na shughuli muhimu zinatalii mawazo haya katika namna mbalimbali.

Uchunguzi kifani ya 3: Kuchora neti katika maumbo tofauti

Bibi Manara alitaka kuendeleza uelewa wa wanafunzi wake kuhusu Hesabu katika maisha ya kila siku na hivyo aliwachukua katika soko lililo karibu. Alichukua karatasi na penseli na kuwataka wanafunzi wake watafute vifaa mbalimbali vya kutilia vitu. Aliwataka wachore michoro rahisi ya vifaa vya maumbo tofauti vya kutilia vitu. Baadhi ya wanafunzi wa Bibi Manara walichora makopo ya tuna ili kuonesha umbo la kisilinda la vifaa vya kutilia vitu na masanduku ili kuonesha mche wa mstatili.

Kwa ajili ya kazi za nyumbani, aliwataka wachore michoro mizuri ya vifaa vya kutilia vitu na jinsi wanavyofikiria neti za maumbo zitakuwaje, kwa kuwa alitaka kuzitundika darasani. Wanafunzi walifurahia sana michoro waliochora na hivyo aliwataka wawakaribishe wazazi wao kuja na kuangalia kazi zao. Bibi Manara alijua kuwa ni muhimu kuwa na ushirikiano mzuri na wazazi, kwa kuwa hali hiyo huboresha ufundishaji mzuri.

Shughuli muhimu: Kutengeneza nyavu za kete

Kabla ya somo, kusanya au tengeneza kete mbalimbali kuonesha darasa lako.

Watake wanafunzi wawili wawili kuangalia kete, na waangalie namba kwa makini –wataweza kutambua kuwa kila sehemu ina namba ya kati ya 1 na 6; unaweza kuwashawishi kuona kuwa sehemu ya pili inajumlisha namba kuwa 7. Wape muda kukagua kama kanuni hii inafuatwa katika kete zao zote.

Sasa wape kila wanafunzi wawili wawili seti mbili za karatasi za mraba fito za 5 x 5. Watake wachore neti tofauti za kete: wavu wa mchemraba wenye namba zilizoandikwa kwenye mraba ili

kufuata kanuni itajwayo hapo juu. Watakapofikiri wamefumbua tatizo, wanaweza kukata nyavu na kuona kama wana kete ‘sahihi’.

Baada ya wanafunzi wawili wawili kuwa wametatua tatizo hili, wanaweza kuweka namba katika kete katika baadhi ya michemraba 11 mingine ambayo wameipambanua.

Watake kila jozi kutengeneza bango kuonesha sulubu ya namba kwa kila wavu.

Unaweza kupanua shughuli hii kwa kuuliza darasa lako kutengeneza ubao wa michezo kuhusu maumbo na kutumia kete zao kuucheza.

Nyenzo rejea 4: Neti Kete yenye namba inaonesha mfano wa jibu sahihi na kiolezo kwa ajili ya wanafunzi wako hodari zaidi ili

Nyenzo-rejea ya 1:  Neti za chuma cha mabati (silinda)