Sehemu ya 3: Kuchunguza maumbo yenye pande 3

Swali Lengwa muhimu: Unawezaje kutumia kazi za vitendo kuchunguza uhusiano wa maumbo ya pandeolwa 2 hadi pandeolwa 3 ?

Maneno muhimu: polihedra; uchunguzi; ruwaza; sura; kingo; vipeo; maumbo yenye pembe nyingi; welewa wa maarifa

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • welewa wako mwenyewe wa maarifa kuhusu pembe nyingi zilizo rahisi za maumbo ya P2 na violwa vya P3;
  • umetalii kazi za vitendo ili kuwasaidia wanafunzi katika kuchunguza uhusiano kati ya maumbo ya pembe nyingi na polihedra.

Utangulizi

Mchakato wa kujenga umadhubuti halisi wa kijiometri unatoa mbinu ya kivitendo na isiyo rasmi kwa wanafunzi kuweza kufahamu na kuelewa violwa vya kijiometri.

Kwa vile wanafunzi wanaweza kugusa maumbo na vitu wanavyojifunza, wanajihisi hali ya kujiamini zaidi katika kufikiri kwa namna dhahania zaidi. Ikiwa maumbo haya yatahusishwa na violwa vilivyomo katika maisha ya kila siku, hii itaboresha kufikiri na ujengaji wa taswira kwa wanafunzi.

Nyenzo-rejea 4: Mfumo wenye namba za kete