Somo la 1

Wakati wa kutalii na kuchunguza polihedra, ni muhimu kuwa na mifano katika darasa lako. Kuna seti mbalimbali za majengo ya plastiki yanayouzwa kwa ajili ya kutengeneza violwa vyenye P3 ambazo zinaweza kununuliwa kwa matumizi ya darasani, lakini ni rahisi pia kutengeneza maumbo yako mwenyewe kwa kutumia violwa vilivyokwishatumika kama vile plastiki, kadi na karatasi nene. Kujitengenezea maumbo yao wenyewe kutawasaidia wanafunzi kuelewa vizuri zaidi tabia za maumbo.

Mirija ya kunywea ya plastiki inaweza kutumika pamoja na uzi na waya kutengeneza ‘viunzi’ vya modeli ya P3. Ukiwa mwalimu, jenga tabia ya kuweka vifaa ambavyo vinaweza kuwa vyenye manufaa darasani –kwa mfano, kuwa na kawaida ya kuhifadhi mrija kila wakati ununuapo kinywaji baridi. Nyavu zilizokwishatengenezwa za ubora mbalimbali ambazo huhifadhiwa kwa kukunjwa, zinaweza kutumika ili kuwasaidia wanafunzi kuchunguza tofauti kati ya maumbo ya P2 na violwa vya P3.

Uchunguzi kifani ya 1: Kutofautisha kati ya violwa vyenye P3 na maumbo yenye P2

Bibi Yomba, mwalimu wa shule ya msingi iliyoko Lindi, Tanzania, alitaka wanafunzi wake wajue tofauti kati ya violwa vyenye P3 na maumbo yenye P2. Alifahamu kwamba somo hili wakati mwingine lilikuwa ni dhana ngumu kwao.

Alivieleza violwa vyenye P3 kama vile ambavyo ‘mtu anaweza kuvichukua, kama vitabu, kalamu, madawati, nk.’ Alisema kwamba maumbo yenye P2 ni vitu unavyoweza kuviona lakini huwezi kuvichukua: taswira ya farasi katika picha, au mchoro wa mtu, hata mraba uliochorwa kwenye karatasi. Alisema, ingawa mtu anaweza kuichukua picha, hawezi kumchukua farasi kutoka kwenye picha au mtu kutoka kwenye mchoro.

Kisha, aliwakaribisha wanafunzi kutaja vitu vingine ambavyo vinaweza kuwekwa katika ama kama P2 au kama P3 darasani. Baadhi ya wanafunzi walihamasika sana kuhusu utofautishaji huo, lakini wengine walihangaika wakiamini kwamba kipande cha karatasi au dirisha ni violwa vya kundi la P3 kwa sababu ni ‘vidogo sana’.

Kisha Bibi Yomba aliamua kuwapa wanafunzi wake kazi ya kufanya nyumbani. Aliwatuma waende nyumbani na kuwaambia wazazi wao kuhusu walichojifunza, na kwamba kazi yao ya nyumbani ilikuwa ni kuleta orodha ya angalau vitu kumi kutoka nyumbani au mazingira ya mahali hapo ambavyo ni violwa vya kundi la P3. Aliamini kwamba kwa kufanya hivi wataimarisha kazi waliyoifanya darasani.

Alifurahia kuona ni wangapi waliweza kutengeneza neti.

Shughuli ya 1: Kufahamu maumbo ya *3D au polihedra

Kabla ya kufundisha somo hili, unahitaji kukusanya au kutengeneza baadhi ya vifaa vyenye 3D na uviweke kwenye boksi (angalia Nyenzo-rejea 1: Maumbo ya rahisi ).

Panga darasa lako katika makundi ya kati ya wanafunzi sita sita na nane nane. Waambie wanafunzi wako waangalie kwa makini maumbo na violwa vilivyomo kwenye boksi. Wauliza wanafunzi wako ni maumbo gani, kama miraba na mistatili, ambayo wanaweza kuyaona kutoka kwenye vitu hivyo.

Waambie majina ya violwa:

Miche mfano, mchemraba, kimchemraba, mcheduara

Piramidi mfano, koni, tufe

Waulize kama wanafahamu violwa vingine ambavyo vinafanana na maumbo haya vilivyoko katika maeneo ya shule au karibu na majumbani kwao.

Eleza kwamba maumbo yote, isipokuwa mcheduara na tufe, vilevile yanaitwa polihedra. Waulize: ‘Unafikiri kwa nini micheduara na matufe hayawekwi katika kundi la polihedra?’ (Angalia Nyenzo-rejea: Kutumia Uelezaji na Uoneshaji katika kusaidia kujifunza kwa ajili ya mawazo ya kukusaidia.)

Waambie wanafunzi kwamba neno polihedron linatoka katika lugha ya Kigiriki lenye maana ya ‘kiti’. Miche na mapiramidi yana sura nyingi bapa kama viti lakini mcheduara si polihedron kwa sababu una ‘sura’ yenye mzingo.

Kamilisha shughuli hii kwa kuwaambia kila kundi kuhesabu sura za kila kiolwa. Waambie waandike rekodi ya majibu yao katika madaftari yao. Kila kundi lishirikishe darasa kwa kuripoti kuhusu majibu waliyotoa.

Kwa ajili ya kazi ya nyumbani, waanbie kama wanaweza kuona maumbo yoyote yanayofanana na haya njiani wanaporudi nyumbani –au nyumbani –na kutoa ripoti siku inayofuata.

Sehemu ya 3: Kuchunguza maumbo yenye pande 3