Somo la 2

Angalia Nyenzo rejea 2: Picha ya piramidi .

Mapiramidi yanawavutia wanafunzi. Hapa tunatalii jinsi ya kujenga picha akilini kuhusu mapiramidi mbalimbali. Mwalimu katika Uchunguzi-kifani 2, kwa kufanya baadhi ya kazi za mitaala tofauti, aliwaonesha wanafunzi wake kwamba hisabati ina uhusiano na masomo mengine na maisha halisi. Shughuli ya 2 inajikita katika hisabati ya mapiramidi kwa kuwataka wanafunzi watengeneze ya kwao wenyewe kwa kutumia nyavu.

Uchunguzi kifani ya 2: Tazama mapiramidi ya karanga ili kuwahamasisha wanafunzi katika hisabati

Wakati Bwana Mtui alipoandaa somo lake, alitaka kuwashirikisha walimu wengine na kuwapa wanafunzi wake zaidi ya uzoefu wa kihisabati peke yake. Alizungumza na wenzake katika kitengo cha maarifa ya jamii na walimpa picha za Piramidi Kuu la Misri (angalia Nyenzo-rejea 2 ).

Alibandika picha mahali ambako wanafunzi wake wote wangeweza kuiona na aliwaambia wamweleze wanaelewa nini kuhusiana na picha hiyo. Bwana Mtui alitengeneza ramani ya maoni ya kitu wanachokijua kuhusu namna mapiramidi yalivyoundwa. (Angalia Nyenzo-rejea Muhimu: Utumiajiwa ramani za maoni na kuchangiana hoja katika kutalii mawazo.)

Kisha, aliwapanga katika makundi madogo madogo ili kujadili kuhusu mapiramidi na kuorodhesha maswali yoyote waliyokuwa nayo kuhusiana na mapiramidi. Aliyakusanya maswali yao yote pamoja na kuchambua yale ambayo yalihusiana na muundo wa mapiramidi na maumbo yake.

Alilipa kila kundi piramidi alilolitengeneza kwa kutumia kadi (angalia Nyenzo-rejea 3: Nyavu za piramidi ). Aliyaambia makundi yafikiri kuhusu umbo na muundo na sifa zozote za jumla –yaani, pande, kingo na sura za kila moja.

Baadaye, aliwaambia wafikiri jinsi watu walivyoweza kujenga miundo mikubwa kama hiyo ya mapiramidi ya Misri. Aliwaonesha picha nyingine zaidi za jinsi mapiramidi yalivyojengwa na jambo hili kwa hakika, lilivutia darasa lake. Matokeo yake, wanafunzi walimwambia mwalimu wao wa maarifa ya jamii awaeleze zaidi kuhusu mapiramidi na Wamisri wa kale.

Bwana Mtui alihisi kwamba mchanganyiko huu wa hisabati na maarifa ya jamii ulisaidia kukuza hamasa ya wanafunzi wakati walipoanza kazi zao za hisabati.

Shughuli ya 2: Kutengeneza mapiramidi ya karatasi

Utahitaji nakala za Nyenzo-rejea 3 , karatasi, mikasi na utepe unaonata au gundi. Ikiwa una vifaa vya kutosha kundi moja tu kufanya kazi kwa wakati mmoja, unaweza kuifanya shughuli hii ifanyike kwa wiki nzima.

Waeleze wanafunzi wako kwamba mapiramidi yanaweza kuwa na vitako vya idadi yoyote ya pande –iliyo rahisi zaidi ya yote ina pembetatu sawa katika nyuso zote nne, lakini mapiramidi yanaweza kutengenezwa kwa kutumia poligoni yoyote ya kawaida kama kitako: mapiramidi ya karanga yametengenezwa kwa pande za pembetatu, lakini yana vitako vya mraba.

Wape nyavu za pembetatu –na mapiramidi yenye vitako vya mraba, na waambie wanafunzi wayakate, wayakunje na kuyatia gundi mapiramidi haya ili kutengeneza mapiramidi ya karatasi. Tundika picha zao.

Kisha, weka baadhi ya mirija au viberiti katika dawati la kila kundi na waambie kama wanaweza, kutumia uzi au utepe unaonata, kutengeneza piramidi kwa kutumia vifaa hivi. Tembea kuzunguka darasa na uyasaidie makundi wakati yakiendelea na kazi. Waruhusu washirikiane kwa kuambiana walichokifanya wakati wa kutengeneza mapiramidi yao.