Somo la 3

Katika sehemu hii, tunaendelea kwenye uchunguzi ulio rasmi zaidi wa maumbo mbalimbali kwa kutumia vitendo ambavyo vinawashirikisha wanafunzi ili wafanye chunguzi makini peke yao kabla ya kutoa baadhi ya tofauti kati ya violwa vya P3. Nyenzo-rejea 4: Violwa vya P3 vinatoa muhtasari unaofaa wa mambo waliyojifunza wanafunzi mpaka wakati huu.

Uchunguzi kifani ya 3: Kutengeneza polihedra zinazotembea

Bibi Mosha alitaka kukuza welewa wa Darasa lake la 5 kwa kujenga baadhi ya maumbo ya polihedra ili kuunda seti mpya zinazotembea za kutundika katika darasa lake. Aliwaambia wanafunzi wake wajigawe katika makundi ya watu sita sita au nane nane, na alilipa kila kundi mikasi, kadi na gundi. Aliliambia kila kundi litengeneze pembetatu sawa 32, miraba 6 na pentagoni 12. Aliandika vipimo vya kila umbo ubaoni.

Aliwaambia wanafunzi wachunguze polihedra ngapi tofauti wameweza kuzitengeneza kwa kutumia poligoni zao, kwa kufuata kanuni hizi:

Tumia aina moja ya poligoni kwa wakati mmoja ili kuunda polihedroni. Polihedroni lazima iwe katika umbo funge. Kingo zote lazima ziungwe. Wanafunzi walifurahia zoezi hili.

Baadaye, aliwapa nyavu za polihedra za kawaida na aliwaambia wazikate vizuri, wazikunje na wazibandike ili kutengeneza polihedra (angalia Nyenzo-rejea 3 ). Waliona kwamba maumbo waliyotengeneza yalikuwa sawa na polihedra walizozigundua.

Alijadili iwapo ilikuwa rahisi zaidi kutumia nyavu kutengenezea polihedra au ni rahisi zaidi kwa kuyaacha maumbo bila kuyafunga. Wanafunzi wengi walikubali kuwa nyavu zilisaidia kazi iende haraka.

Shughuli muhimu: Sifa za maumbo rahisi ya P2 na violwa vya P3

Kwanza, kazia ujifunzaji wa wanafunzi kutoka katika shughuli zilizotangulia. Ili ufanye hivi, utahitaji boksi lako la maumbo na violwa na chati za kurekodia matokeo (angalia Nyenzo-rejea 5: Kuandika matokeo ) au waambie wanafunzi wako wachore chati mbili katika madaftari yao.

Wapange wanafunzi wako katika jozi au makundi madogo madogo. Wapo kifaa kimojawapo kutoka katika boksi lako la maumbo, na waambie waangalie kwa makini maumbo haya na wakamilishe chati kwa ufasaha kadri wawezavyo.

Washauri wakamilishe mstari mmoja mmoja kwa wakati. Waambie warudishe maumbo kwenye boksi, na wachukue umbo lingine mpaka watakapokuwa wameangalia maumbo yote.

Baada ya muda utakaotumika kwa kazi hito, iambie jozi moja au kundi kutoa majibu yao ya umbo moja mbele ya darasa. Tembea kuzungukia darasa mpaka sifa za maumbo yote zimefahamika kwa kila kundi, na kila jozi imeweza kukagua majibu yao kwa kuyalinganisha na ya wengine.

Waulize kama wamegundua ruwaza zozote katika chunguzi zao. Maumbo na violwa gani vinahusiana? 

Onesha chati zao.

Unaweza kutaka kutumia mchezo wa ‘Pambano la Nafasi’ katika

Nyenzo-rejea 5 kukamilisha mada hii, na tathmini welewa wao wakati wanacheza. Unaweza kuligawa darasa katika timu ili kucheza mchezo huu.

Unaweza kuhitaji kutumia vipindi viwili kwa shughuli hii.

Nyenzo-rejea ya 1:  Kukusanya na kutengeneza maumbo na violwa