Sehemu ya 4: Kuchunguza ulinganifu

Swali Lengwa muhimu: Unawezaje kutumia violwa vya kila siku katika kukuza welewa‘dhahania’ wa ulinganifu kwa wanafunzi?

Maneno muhimu: mistari ya ulinganifu; uakisi; mzunguko; asili; maswali sifunge;mitaala kingamo

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • umetumia kazi za vikundi katika kusaidia ukuzaji wa welewa wa wanafunzi kuhusu ulinganifu na mifumo mingine ya mizunguko linganifu;
  • kujenga mikakati anuwai ikiwa ni pamoja na utumizi wa maswali sifunge katika kukuza ujuzi wa kufikiri kuhusiana na;
  • ulinganifu; umeshughulikia sehemu mbalimbali za mtaala ili kukuza maarifa kuhusu ulinganifu.

Utangulizi

Kama ukikunja ukurasa usio na maandishi katika nusu na kuukunjua tena, kila upande wa mkunjo utaonekana kama uakisi wa sehemu moja kati ya mbili hizo. Zinapokunjwa, pande hizo mbili hupishana na kufunikana sawasawa. Uakisi huu ni linganifu. ‘Kioo’ au mstari wa ‘mkunjo’ ambavyo vinasababisha uakisi sawa wa pande hizo mbili unaitwa mstari wa ulinganifu.

Maumbo mengi ya kihisabati yana mistari ya ulinganifu, na viumbe vingi vyenye uhai vinakadiriwa kuwa na umbo lenye ulinganifu. Sehemu hii itakusaidia kukuza welewa wako kuhusu ulinganifu, na kujaribu mikakati anuwai ya kufundisha kuhusu mada hii.

Nyenzo-rejea 5: Kuandika matokeo