Somo la 2

Pamoja na kuwahamasisha wanafunzi kuangalia ulinganifu katika ulimwengu unaowazunguka, mada hii inawawezesha wanafunzi kuwa wabunifu na kutengeneza vitu na sampuli zenye ulinganifu. Ni fursa nzuri kufurahia kazi za mitaala anuwai katika sanaa. Shughuli hizi zinaweza kufanywa na wanafunzi wadogo sana, bado zikawa shughuli sifunge kiasi kwamba hata wanafunzi wakubwa zaidi wanaweza kuzikuza wenyewe.

Uchunguzi kifani ya 2: Kuunda vipepeo wenye ulinganifu

Bibi Ngetu alitaka kutumia sanaa katika kuwasaidia wanafunzi kutalii ulinganifu na aliamua kutumia kipindi kwa kutengeneza picha za kipepeo na wanafunzi wake. Alitafuta picha mbili za vipepeo, ambazo alizionesha darasani kwake. Alieleza jinsi kipepeo alivyo na mabawa manne, na jinsi ukubwa ulivyokuwa unatofautiana, umbo na rangi za mabawa hayo zinavyoweza kuwa, lakini mabawa na sampuli zake kwa kawaida ni linganifu.

Kwa kukunja kipande cha karatasi, Bibi Ngetu alilionesha darasa jinsi ambavyo angekata umbo la bawa la kipepeo, angefungua ukurasa, na kuwa na jozi ya mabawa ya kipepeo. Vile vile, aliwaonesha jinsi ambavyo wangeweza kuunda sampuli za vipepeo kwa kukunja karatasi yenye mpako mbichi wa gundi kwa ndani. Aliwapa nafasi wanafunzi ili watengeneze vipepeo wao wenyewe, huku wakikumbuka maumbo mbalimbali ya mabawa na sehemu mbalimbali. Wanafunzi wadogo walitumia kalamu za rangi katika kupaka rangi vipepeo wao, wakati wanafunzi wakubwa walichora ruwaza tatanishi za mistari linganifu.

Wakati vipepeo walipokamilika, Bibi Ngetu aliwatundika kwenye paa la darasa kwa kutumia kamba. Wanafunzi wake walipata msisimko walipowaangalia na walizungumza sana kuhusu sampuli hizo.

Shughuli ya 2: Vinyago linganifu

Utahitaji penseli na kalamu za kutosha au rangi ili kila mwanafunzi atengeneze kinyago cha kuvutia, kamba au kamba ya mpira kwa ajili ya kuning’inizia vinyago, na vipande vya kadibodi vikubwa kiasi cha kutosha kutengenezea vinyago. Utahitaji kutumia muda wa kutosha katika kukusanya vitu hivi kabla ya kuanza shughuli hii lakini wanafunzi wako wanaweza kukusaidia kukusanya zana pamoja (angalia Nyenzo rejea: Kuwa mwalimu mbunifu katika mazingira yenye changamoto ).

Waeleze wanafunzi kwamba watatengeneza vinyago, lakini vyote viwili, umbo la kinyago na mchoro au picha ya kuchora yoyote ile, lazima viwe linganifu. Pendekeza kwamba watengeneze maumbo ghafi ya awali kabla ya kuanza kazi kamili. Unaweza kuwaonesha baadhi ya vinyago vya mahali hapo. Labda wanaweza kukusanya vifaa vya kufanyia kazi na kutengeneza maumbo ghafi ya awali katika kipindi kimoja, na kutengeneza kinyago kamili katika kipindi kimoja au viwili vitakavyofuatia.

Pendekeza watengeneze vinyago vya watu, majani, wanyama, mabawa, viumbe wa kufikirika, au vinyago vya kikabila. Huu uwe uamuzi ambao utamwachia kila mwanafunzi aamue, au amua kitu kimoja kwa darasa zima.

Tafakari kuhusu vifaa gani unavyoweza kuwasaidia wanafunzi katika kuumba vinyago vyao (kama vile picha au violwa –angalia Nyenzo rejea 2: Mifano ya ulinganifu katika vinyago vya Kiafrika ). Shughuli gani nyingine za kibunifu zinaweza kufanywa na wanafunzi ili kukazia welewa wao wa ulinganifu?