Somo la 3

Kwa kiasi Fulani, uhamishaji ni shughuli rahisi, kwa sababu inaathiri viwianishi vya vipeo vyote kwa namna moja (kwa mfano, viwianishi vyote vya x vitaongezeka au kupungua kwa kiasi sawa).

Uakisi ni changamani zaidi kihisabati, kwa sababu ni lazima ukiangalie kila kiwianishi kwa utofauti wake na wakati huo huo kwa kukihusisha na kitu kingine –mahali pa mstari wa kioo. Kwa hiyo, uakisi unahitaji wanafunzi kufahamu idadi kubwa ya dhana akilini mwao katika wakati mmoja (angalia Nyenzo-rejea 4 ).

Fikiri kuhusu mifano ya kawaida ya uakisi ambayo unaweza kuitumia ili kuwasaidia wanafunzi wako katika mada hii –labda baadhi ya kazi ambazo unaweza kuwa umeshazifanya katika ulinganifu au sampuli na mitindo ya sanaa itumiayo dhana za kijadi za mahali hapo. Tafakari kuhusu jinsi wanafunzi wanavyoweza kutumia maumbo yaliyokatwa kadri wanavyokuza uwezo wao wa kushughulikia maumbo hayo kiakili.

Zaidi ya hapo, sehemu hii inashauri kwamba uendelee kuwahimiza wanafunzi wajadili tafakuri zao –ufunguo muhimu katika kufungua welewa wao wa hisabati.

Uchunguzi kifani ya 3: Utumiaji wa kazi za vikundi ili kusaidia kutafakari kuhusu uakisi

Bibi Nkony, mwalimu mzoefu katika shule ya msingi iliyoko Kilimanjaro, amefundisha misingi ya uakisi katika darasa lake. Sasa anaamua kuwasaidia wanafunzi kujadili shughuli na matokeo yao.

Anafahamu kwamba mjadala sio tu unahusu kujibu maswali mafupi au funge, kwa hiyo anaamua kuandaa utaratibu ili kusaidia mjadala miongoni mwa wanafunzi wake. Anawapanga katika jozi. Wanaambiwa waangalie kazi za kila mmoja, na kufanya uchunguzi wa aina tatu kuhusu uakisi ambao watauripoti baadaye. Kwa kila uchunguzi, lazima wote wafurahie kwamba wamepata namna ya kuuelezea au kuufafanua kwa ufasaha kadri wawezavyo. Wakati wanakikundi wote wawili watakapokubaliana kwamba wana uchunguzi wa namna tatu, wanyooshe mikono yao juu.

Kisha, Bibi Nkony anaziweka jozi pamoja ili kuunda kikundi cha watu wane, na kuwaambia kila jozi kuelezea uchunguzi wao kwa jozi nyingine. Baadaye, anawaambia wanafunzi hao wanne waamue kuhusu chunguzi tatu bora au zinazovutia zaidi ili kuzitolea ripoti darasani.

Anagundua kwamba anaweza kutumia mbinu hii ya kazi katika masomo mengine mbali ya hisabati. Ili kufahamu kuhusu kitu gani wanafunzi wako wanafahamu na wanaweza kufanya angalia Nyenzo-rejea Muhimu: Kutathmini Ujifunzaji .

Shughuli muhimu: Kutafakari kuhusu uakisi

Wanafunzi wanaweza kutumia tena maumbo waliyoyakata katika karatasi ya fito mraba ya Shughuli ya 2 , au watengeneze mengine kama ni muhimu kufanya hivyo.

Kwenye kipande cha pili cha karatasi ya fito mraba, waambie wanafunzi wachore na kuweka alama ya mihimili ya x-y yenye urefu wa angalau miraba (angalia Nyenzo-rejea 4 ).

Ili kuweka mojawapo kati ya maumbo yaliyokatwa kwenye karatasi kwa kusudi la kuzifanya kona zake ziwe kwenye ‘misalaba’ ya fito mraba, lazima waoneshe vipeo (a, b, c na d kama inavyostahili), kisha wachore umbo hilo na kuandika viwianishi vya kila kipeo (kona).

Waambie wanafunzi wachore mstari wa kwenye kioo wa wima au ulalo katika fito miraba zao. Kisha, lazima wachore uakisi wa umbo kwa upande wmingine wa mstari wa kioo (wakumbushe wanafunzi kwamba wanaweza kutumia umbo lilikatwa kama inawawia rahisi) na waandike viwianishi vya uakisi.

Wape changamoto wanafunzi wako kushughulikia viwianishi akisi bila kutumia umbo lililokatwa. Waambie wafafanue jinsi walivyofanya. Wafanyishe mazoezi kwa kutumia maombo mengi ili waweze kujenga hali ya kujiamini.

Ulifanikiwa vipi kutambulisha na kuelezea shughuli hii? Unajuaje hili?

Nyenzo-rejea ya 1: Baadhi ya mitindo ya vitambaa vya Kitanzania