Somo la 1

Kutumia ramani ya mawazo kutakusaidia kutambua nini wanafunzi wako wanajua tayari kuhusu kipimo katika maisha ya kila siku. Taarifa hii itakusaidia kupanga shughuli ambazo zitaendeleza uelewa wao zaidi. Angalia Nyenzo muhimu: Kutumia ramani za mawazo na kushirikishana mawazo kuchunguza dhana kwa njia za kufanya hivi.

Nyenzo rejea 1: Ramani ya mawazo ya kipimo inaonyesha mfano wa ramani ya kumbukumbu ya dhana ya kundi moja .

Uchunguzi Kifani 1: Tambua wanafunzi wako wanachofahamu

Bi Lekani, aliyeko Nigeria, alitaka kutambua wanafunzi wake walichokuwa wanafahamu tayari juu ya kipimo katika maisha ya kila siku. Alishatumia nao ramani zamawazo kabla, hivyo wanafunzi walikuwa si wageni wa wazo hilo. (Angalia Nyenzo muhimu: Kutumia ramani za mawazo na kushirikishana mawazo kuchunguza dhana .

Aliwagawa wanafunzi katika makundi ya watano watano, aliyapa makundi mwelekeo kwa ramani za mawazo yao: kwa baadhi, alisema ‘muda’ kwa wengine ‘umbali’ kwa wengine ‘uzito’.

Aliwaambia kila kundi kukamilisha ramani ya mawazo kuonyesha yote waliyoweza kufikiria kulingana na mada zao maalumu; aliwakumbusha wafikirie maeneo yote tofauti ambayo wangeweza kukutana nayo kwenye kipimo- nyumbani, shuleni, sokoni. 

Baada ya kuwa wamelifanyia kazi hili kwa muda wa kama dakika 15, aliliambia kila kundi likiwa na fokasi/ msisitizo wa mada hiyohiyo kuonyesha ramani za mawazo yao pamoja.

Alitoa dakika kumi kwa darasa zima kuangalia ramani za mawazo na kujadili kufanana na kutofautiana kwazo. Aliorodhesha mifanano na kuitumia kama msingi wa kupanga kazi zaidi kwa kila eneo.

Shughuli ya 1: Kutumia ramani ya mawazo kwa kipimo

Kama hujatumia ramani za mawazo kabla, soma Nyenzo muhimu: Kutumia ramani ya mawazo na kushirikishana mawazo kuchunguza dhana. Jaribu kuchora ramani yako ya kumbukumbu ya somo ulilofundisha karibuni, kujizoesha na utaratibu.

Anza somo lako kwa kujadili ramani za kumbukumbu na namna zinavyofanya kazi. Halafu, yaambie makundi yafanye kazi kwa dakika 15 kwenye ramani za kumbukumbu zao wenyewe juu ya kipimo. Waweke pamoja na waonyeshe ramani zao za kumbukumbu (angalia Nyenzo rejea 1 kwa ajili ya mfano) au kwa mara ya kwanza ungeweza kufanya ramani ya kumbukumbu ya darasa ambapo unaandika dhana zinazopendekezwa na wanafunzi wako.

Jadiliana na darasa zima kufanana na kutofautiana kati ya ramani za kumbukumbu. Dhana zipi ni za kawaida?

Waambie wanafunzi waeleze dhana yoyote ambayo haieleweki vizuri na waambie wafikirie maswali waliyonayo kuhusu kipimo. Yaorodheshe pamoja na maeneo waliyotambua kama muda, umbali n.k.. Haya yatakusaidia kupanga hatua zitakazofuata.

Baada ya somo, andika njia zote unazofikiri ramani za mawazo zinaweza kusaidia kufundisha kwako na kujifunza kwa wanafunzi wako. Angalia Nyenzo rejea 2: Namna gani ramani za mawazo zinaweza kuwasaidia waalimu wa hisabati nawanafunzi ili kupata mawazo. Kwa kuwa zimeorodheshwa, ni matumizi gani ya vitendo yamefanyika kwa kuziandika wewe mwenyewe?

Sehemu ya 1: Kuwasilisha vipimo