Somo la 2

Fikiria kumuuliza mwalimu wa sayansi akusaidie kuwaonyesha wanafunzi namna ya kupima mapigo ya myoyo yao au fanya wewe mwenyewe kwa kutumia Nyenzo rejea 3: Kiasi cha moyo ili kupata msaada. Huu ni utangulizi mzuri kuelekea kwenye kipimo halisi, kwa kuwa inaweza kufanyika bila kutumia kifaa chochote zaidi ya saa moja ya mkononi kwa ajili ya kutumiwa na mwalimu au mwanafunzi. Kinaweza pia kujumuishwa na baadhi ya mazoezi ya kufurahisha na shughuli za kujirudia, na kutoa msingi mzuri wa kazi ya mtaala tambuka, kwa mfano, wiki ya ‘miili yenye afya’. Shughuli za vitendo kama hii itateke usikivu wa wanafunzi pamoja na kuwahusisha.

Nyenzo rejea 3 inakuambia namna ya kupima mapigo ya moyo, na inatoa habari zaidi kuhusu mapigo ya moyo, umri na zoezi la kukusaidia kwa Shughuli 2.

Uchunguzi kifani ya 2: Kupima mapigo ya moyo

Bi Lekani aliwaeleza wanafunzi wake namna ya kupima mapigo yao ya mioyo kwa kushikilia vifundo vya mikono ya kushoto kwa vidole vya katikati vya mikono ya kulia na kuhesabu mapigo ya mishipa ya damu. Aliwaambia wafanye hivi kwa dakika chache. Wanafunzi walifurahia sana kufanya hivi- hakuna hata mmoja aliyehisi mapigo ya mishipa kabla. Bi Lekani alihakikisha kuwa kila mwanafunzi alipata pigo la mshipa, iwe shingoni au kwenye kifundo cha mkono. Wote walipima mapigo ya mishipa wakiwa wamekaa na waliliandika hili, au walilikumbuka.

Halafu aliwaambia wasimame na kukaa chini haraka haraka mara kumi na kusikilizia mapigo ya moyo tena. Wanafunzi walishangazwa kuona kuwa mapigo yaliongezeka kasi. Aliwaambia wahesabu mapigo ya moyo kwa sekunde kumi na kuzidisha mara 6 ili kupata kiasi cha mapigo kwa dakika.

Bi Lekani aliwaambia wanafunzi wafikiri kwanini haya mabadiliko yangeweza kutokea na kuorodhesha mawazo yao ubaoni, kwa mfano, walihitaji nguvu zaidi. Alifurahishwa na fikira zao na aliona wakijaribisha hili kiwajani wakati muda wa mapumziko.

Shughuli ya 2: Kupima kiasi cha mapigo ya moyo baada ya zoezi

Kabla ya somo kuanza, hakikisha kuwa unaweza kupima kiasi cha mapigo ya moyo shingoni kwako au kwenye kifundo cha mkono (angalia Nyenzo rejea 3 ). Jaribu kwa kuwaonyesha marafiki na familia yako jinsi ya kufanya hivi kabla hujafanya darasani!

Waonyeshe wanafunzi wako namna ya kuhisi mapigo ya mishipa shingoni na kwenye kifundo cha mkono, na hakikisha kuwa kila mwanafunzi anaweza kuhisi mapigo ya moyo angalau kwenye moja kati ya maeneo haya kwa kutumia kidole cha kati.

Anza somo kwa kuwaambia wanafunzi wako kuwa wanaenda kufanya jaribio. Wakati wa jaribio inabidi wakae kimya watulie kabisa.

Kutumia saa yako (au saa yoyote ya ukutani ionyeshayo sekunde), waambie wanafunzi watafute mapigo ya mishipa, halafu wahesabu mapigo mangapi wanahisi kwa muda wa dakika moja. Waambie waandike kiasi cha mapigo ya moyo lakini wasiongee.

Baada ya hapo, fanya mazoezi ya kawaida (kwa mfano kutembea kwa muda wa dakika mbili) kisha waambie wapime mapigo ya moyo tena.

Subiri kwa dakika moja na waambie wapime tena. Hifadhi matokeo

Wangeweza wakafanya zoezi lingine, kwa mfano kuruka au kukimbia, na kisha kupima mapigo ya moyo tena na kuhifadhi matokeo.

Waambie wanafunzi wote waorodheshe ubaoni mapigo ya mioyo yao baada ya kutembea na kuruka.

Jadiliana nao juu ya matokeo tofauti waliyonayo kwa kila shughuli: kwa mfano, kwa nini mapigo yalikuwa juu baada ya kuruka kuliko kutembea?