Somo la 3

Kuelewa umuhimu wa ‘kizio’ na uwezo wa kusoma vigezo ni vya maana kwa kazi ya kufaa ya kipimo. Sehemu zinazofuata katika moduli hii zitashughulika na urefu, uzito na muda: kwa kila kimoja, ni muhimu kwa wanafunzi kuelewa kizio sahihi, na namna ya kusoma kwa usahihi vigezo vya vifaa vya upimaji. Sehemu hii inaangalia jinsi unavyoweza kupanga shughuli kuwasaidia wanafunzi kuendeleza ustadi huu. Kwa kutumia shughuli kwa vitendo zinazohusiana na maisha yao ya kila siku, wanafunzi wataona lengo kwenye kazi na watavutiwa zaidi.

Uchunguzi kifani ya 3: Kupanga hatua zitakazofuata kwa ajili ya uelewa wa wanafunzi wa kupima

Bi Chifupa alishatumia muda kufanyia kazi vizio tofauti vya kupima na wanafunzi wake. Alihisi kuwa sasa walikuwa wanajiamini katika kusoma vigezo kwenye rula zao, na kusoma vigezo vya uzito alivyoleta kutoka nyumbani kwake. Walishaongelea juu ya sentimita na milimita na waliweza kuvionyesha kwenye rula zao, na kueleza uhusiano kati yake. Walijua umbali kati ya miji na kwamba huu ulipimwa kwa kilometa. Bi Chifupa alifurahishwa na maendeleo yaliyofikiwa, na alitaka kuhakikisha kuwa wanafunzi sasa wangeweza kuona ’mili-‘ ‘senti-‘ na ‘kilo-‘ zikitumika kwenye vipimo vyote na vizio. (Angalia Nyenzo rejea 4: Vizio vya kipimo .)

Aliamua kufanya hivi kwa kutumia vipimo ‘visivyo na maana’- kutengeneza vizio vya mchezo, na kuuliza maswali juu yake (angalia Nyenzo rejea 5: Nafasi na kupima kama mfano wa maswali yasiyo na maana). Baada ya wanafunzi wake kushika kile alichokuwa anafanya, aliwaambia watengeze maswali yao wenyewe ya kupima yasiyo na maana, ambayo waliyafurahia sana. Bi Chifupa alikuwa na uhakika kuwa mwishoni walijua vema maana ya ‘mili-‘, ‘senti-‘ na ‘kilo-‘, kwa sababu walikuwa na uwezo wa kueleza tofauti zake kwenye majadiliano.

Shughuli muhimu: Kupanga somo la uchunguzi kuhusu kipimo

Panga shughuli hii angalau na mwalimu mwingine mmoja shuleni kwako.

Tengeneza orodha ya vifaa vyote vya kupimia unavyoweza kuvipata na kuletwa shuleni (kama vile rula, vipima uzito/mizani, jagi la kupimia au kijiko). Vifaa vyenye vigezo ni vizuri zaidi. Ni vipi watu wauzao mboga sokoni hupima kile wateja wao wanachotaka? (Kwa ushauri wa jinsi ya kukusanya zana, angalia Nyenzo muhimu: Kuwa mwalimu mwerevu kwenye mazingira yenye changamoto .)

Fikiria shughuli ambazo zitawaruhusu wanafunzi kujaribisha kutumia vifaa hivi na kuweka kumbukumbu za vipimo, kukuza kujiamini na usahihi.

Fikiria namna utakavyowasilisha maneno muhimu: vizio, kipimo, kigezo, umbali, uzito, ujazo, muda, na nini wanafunzi wako watafanya kuelewa na kukumbuka manano haya.

Amua jinsi utakavyowapanga wanafunzi wako, muda gani utaruhusu na zana utakazohitaji ili kufanya shughuli hizi.

Panga somo lako, ukihakikisha kuwa, pamoja na kuweka kumbukumbu ya ‘idadi’ kutoka kwenye kifaa au kigezo, wanafunzi pia waweke kumbukumbu za vizio na nini kinachopimwa (kwa mfano umbali, uzito, ujazo, muda). Angalia Nyenzo muhimu: Kupanga na kuandaa masomo yako .

Fanya somo hili. Kama inawezekana, mwombe mwalimu aliyekusaidia kuandaa shughuli kusimamia sehemu au somo lote, na baadaye ajadiliane na wewe juu ya somo hilo. Nini kilienda vizuri? Nini kilikuwa kigumu? Wapi kuna matokeo yasiyotarajiwa? Ni vipi ungetathmini uelewa wa wanafunzi wako wa jinsi ya kupima?

Nyenzo-rejea ya 1: Ramani ya mawazo ya kipimo