Nyenzo-rejea ya 2: Namna gani ramani za mawazo zinaweza kuwasaidia waalimu na wanafunzi wa hisabati
Taarifa za msingi/welewa wa somo wa mwalimu
Ramani za mawazo zinaweza kuwasaidia waalimu wa hisabati:
- Kupanga mada na masomo katika njia yenye mantiki na ya utaratibu mzuri;
- Kung’amua na kupanga shughuli;
- Kuanzisha dhana mpya kwa wanafunzi katika njia inayovutia;
- Kuwezesha uelewa mzuri wa dhana;
- Kuelekeza uangalifu wa wanafunzi kwenye dhana muhimu za mada;
- Kusaidia wanafunzi kujiandaa kwa majaribio na mitihani;
- Kuratibu taarifa ambazo wanafunzi wana uwezo wa kuzitambua na kujihusisha nazo;
- Kusaidia kutambua dhana zisizo sahihi za wanafunzi;
- Kutathmini uelewa wa wanafunzi wa dhana na mada;
- Kupanga msaada zaidi kwa baadhi ya wanafunzi.
Kwa sababu ramani za dhana/mawazo zinaweza kuchorwa na wanafunzi wenyewe, ni vifaa muhimu kwa elimu inayomlenga mwanafunzi.
- Ramani za Mawazo zinaweza kuwasaidia wanafunzi:
- Kujumuisha elimu juu ya mada na kutoa maelezo ya jumla;
- Kupangilia mada kulingana na umuhimu wake na uhalisia;
- Kuunganisha mawazo mapya na vitu walivyojifunza mwanzoni;
- Kuonyesha elimu awali ya mada;
- Kupunguza wasiwasi ili wanafunzi wajue nini cha kusoma na nini cha kuacha.
Nyenzo-rejea ya 1: Ramani ya mawazo ya kipimo