Somo la 2

‘Baadhi ya watu wanaweza kutaja muda kwa kuangalia jua. Lakini sijawahi weza kuweka namba’.

Unaweza kuona ni msaada kumshirikisha mwalimu wa historia kuangalia namna muda ulivyokuwa unapimwa katika tamaduni tofauti katika historia. Hii ingeweza kuwa ni shughuli- wanafunzi wako huenda wakafurahia kujaribu baadhi ya hizi njia za zamani za kutaja muda, kama vile kutengeneza saa za mishumaa au saa za vivuli. Itawaonyesha wanafunzi wako kuwa hisabati ni –na daima itakuwa- muhimu katika maeneo mengi ya maisha na kujifunza.

Kutumia wataalamu wengine darasani kwako kutakusaidia kujifunza zaidi kuhusu somo hili na kuwapa motisha wanafunzi wako. Mwalimu katika uchunguzi kifani 2 anatumia mbinu hii.

Uchunguzi kifani ya 2: Kutumia wataalamu wengine kusaidia kufundusha muda

Bi Tokunbo alitaka kuwafundisha wanafunzi wake kuhusu muda. Alianza kwa kuwahadithia hadithi za namna watu katika kijiji cha baba yake walitaja muda wa siku na jinsi walivyojua kupangilia sharehe na matukio. Aliwauliza kama walifahamu namna urefu wa kivuli wa mlingoti ulivyotumika kutambua muda wa kufanya shughuli fulani na muda wa Waislamu wa kufanya maombi.

Bi Tokunbo alimwomba mwalimu wa historia asaidie kwa kueleza jinsi muda ulivyokuwa unapimwa hapo zamani. Mwalimu wa historia aliwaeleza juu ya ndege wanaolia katika vipindi fulani vya mchana au usiku, kama jogoo ambao huwika asubuhi, na uhusiano kati ya misimu ya miaka na kiangazi na vipindi vya kupanda na kuvuna. Aliwaeleza jinsi baadhi ya watu walivyotumia mwezi kutaja muda wa mwezi mzima.

Kwa kumshirikisha mwalimu wa historia, Bi Tokunbo aliwaonyesha wanafunzi wake kuwa hisabati sio somo lililojitenga, na yeye mwenyewe alijifunza baadhi ya mifano mipya na mawazo juu ya muda ambayo hukujua. (Angalia Nyenzo rejea 1, 2 na 3 kwa baadhi ya mifano.)

Shughuli ya 2: Kupima muda kwa kutumia saa ya kivuli

Kabla ya somo, kusanya baadhi ya vijiti na chaki. Ungeweza pia kusoma Nyenzo rejea 3 kujifunza zaidi juu ya saa za vivuli.

Waonyeshe wanafunzi saa za vivuli na namna zinavyofanya kazi. Liambie kila kundi la wanafunzi litengeneza saa rahisi ya kivuli kwa kutumia kadi, penseli au kijiti na tope kidogo (au weka kijiti ardhini).

Tumia tope kushikilia kijiti juu ya kadi, na weka saa ya kivuli kwa nje. Waambie wanafunzi waweke alama ya kivuli kwa vipindi fulani katika siku- ‘shule ikianza’, somo la hisabati likianza’, ‘muda wa mapumziko’, ‘muda wa chakula cha mchana’, na kuendelea kwa siku nzima.

Mwishoni mwa siku, linganisha nyuso za saa. Jadili jinsi kivuli kilivyokuwa kikitembea. Wanafunzi wanaweza kueleza ni kwa nini?

Wangeweza kujifanya wao wenyewe kuwa saa za vivuli kwa kusimama sehemu moja kwa vipindi fulani mchana na kuona nini kinatokea kwenye vivuli vyao. Waambie wachangie majibu yao na waorodheshe mabadiliko waliyoyaona kuhusu vivuli vyao.