Somo la 3

Kuna mambo kadhaa muhimu ambayo wanafunzi wanapaswa kujua kuhusu muda (angalia Nyenzo rejea 4: Vizio vya muda ), lakini moja kati ya vitu vinavyotia changamoto kwa wanafunzi wadogo mara nyingi ni kuweza ‘kusoma’ uso wa saa. Matumizi ya shughuli za vitendo za ‘saa za mikono’ yawasaidie wanafunzi waweze kusoma saa na kutaja muda.

Pindi unapokuwa na saa, anza na mida ambayo ni rahisi, taratibu ukienda kwenye mida migumu:‘katika saa’ (kamili);robo, nusu, saa, kasoro robo; muachano wa dakika tano tano; muachano wa dakika moja moja.

Uchunguzi kifani 3 na shughuli muhimu vinatoa mifano ya namna unavyoweza kufanya hili.

Uchunguzi kifani ya 3: Kutaja muda

Bi Afolabi alitaka wanafunzi wake waweze kurekebisha na kusoma muda mbalimbali kutoka kwenye uso wa saa. Aliamua kitu kizuri cha kufanya kilikuwa ni kuwaambia wanafunzi saa za vipande vya kadibodi. Aliwaambia wanafunzi wamsaidie kukusanya kadibodi nyingi ili kila kundi la wanafunzi waweze kutengeneza saa kubwa na mikono yake miwili.

Walipokusanya vya kutosha, aliwaambia wanafunzi wake wakate nyuso za duara na mikono kutoka kwenye kadibodi zao; na aliwaonyesha namna ya kuweka namba kwenye bodi, akihakikisha kuwa walikuwa na 12, 3, 6, na 9 katika asehemu muhimu. Bi Afalobi alikuwa amenunua baadhi ya pini kwa ajili ya kushikisha mikono kwenye nyuso za saa.

Bi Afolabi baadae aliwaelezea wanafunzi wake namna wangeweza kutumia saa, kwa kuanza na kutaja masaa, (saa saba kamili n.k). Aliwaonyesha wanafunzi muda maalumu kwenye saa yake aliyoitengeneza nao walifuatishia muda huo. Walifanya kazi katika makundi madogo, wakisaidiana. (Angalia Nyenzo muhimu: Kutumia kazi za vikundi darasani kwako .)

Walitumia saa walizotengeneza kwa wiki/majuma kadhaa, hadi hapo Bi Afolabi alipohakikisha kuwa wanafunzi wake wote wangeweza kutaja muda kwa kujiamini. Kila siku, alileta pia darasani saa ndogo ya kengele. Aliiangalia saa hii na wanafunzi wake katika vipindi tofauti vya siku kuona ni muda gani ulikuwa.

Shughuli muhimu: Kutaja muda

Kusanya vifaa na tengeneza nyuso za saa za kadibodi na wanafunzi wako.

Anza kwa kufundisha darasa zima ili kuwasaidia wanafunzi waone jinsi saa na dakika zinavyokuwa.

Wanafunzi wanapokuwa hawana tatizo na hili, unaweza kuwaambia wakiwa wawili wawili au kwenye makundi madogo kushindana wao kwa wao; iwe kwa kutaja muda na kuwaambia wenzao wauonyeshe kwenye saa, au kuweka muda kwenye saa na kuwaambia wenzao waseme ni muda gani unaoonyeshwa.

Waambie, wakiwa kwenye makundi, watengeneze orodha ya vitu muhimu wanavyofanya kwa siku, ikiwa ni pamoja na muda wanaofanya vitu hivyo. Unaweza kuwasaidia wanafunzi wadogo. Ungeweza kutengeneza picha ya muda.

Mwishoni mwa somo, au kwenye somo linalofuata, waambie wachore nyuso za saa kwenye daftari zao, waonyeshe muda na kuandika muda kwa maneno kwa kila saa. (kama unaweza, uwe na kitu kimoja au viwili vya duara ambavyo wanafunzi wanaweza kutumia ili kuokoa muda.)

Fanya somo hili. Kama inawezekana, mwombe mwalimu aliyekusaidia kuandaa shughuli kusimamia sehemu au somo lote, na baadaye ajadiliane na wewe juu ya somo hilo. Nini kilienda vizuri? Nini kilikuwa kigumu? Wapi kuna matokeo yasiyotarajiwa? Ni vipi ungetathmini uelewa wa wanafunzi wako wa jinsi ya kupima?

Nyenzo-rejea ya 1:Njia zilizotumika kupima muda zamani