Nyenzo-rejea ya 1:Njia zilizotumika kupima muda zamani

Nyenzo rejea ya mwalimu kwa ajili ya kupanga au kurekebisha ili kutumia naWanafunzi

Hadithi ya kutumia kuwika kwa jogoo kutaja muda

Bwana Adebowale ni mfanyabiashara mdogo wa kijijini. Hupeleka bidhaa zake vijiji vya jirani siku za masoko. Kwa kawaida hutembea kwa miguu kwenye vijiji hivyo. Ili kujua muda wa kuanza safari, alikuwa akisikiliza kuwika kwa jogoo asubuhi na mapema; hii ilimtambulisha kuwa kumekucha na alianza safari. Lakini siku moja, jogoo aliwika mapema sana. Bwana Adebowale alidhani kuwa kumekucha na alianza safari. Alipokuwa anaingia barabarani, aliona kuwa ilikuwa bado giza sana na kwa muda mrefu alisafiri peke yake gizani. Vilevile alifika sokoni mapema sana na ilibidi asubiri kwa muda mrefu kabla watu wengine hawajafika. Tangu siku hiyo, Bwana Adebowale alihitimisha kuwa kutegemea kuwika kwa jogoo kujua kama kumekucha sio sahihi mara zote

Nyenzo-rejea ya 2: Saa za maji – njia za kupima muda katika historia