Sehemu ya 4: Kupima uzito

Swali Lengwa muhimu: Ni namna gani unaweza kufundisha kupima uzito kwa kutumia njia za vitendaji/matendo na Nyenzo rejea rahisi?

Maneno muhimu: vipimo sanifu; gramu; kilogramu; kazi zinazowezekana; uwiano;

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • kuwasaidia wanafunzi kuelewa uzito kwa kutumia shughuli mbalimbali;
  • kuwawezesha wanafunzi kuelewa hitaji la kutumia vipimo sanifu vya uzito;
  • kutumia njia mbalimbali kuandaa darasa lako.

Utangulizi

Mnapochunguza uzito na wanafunzi, ni vema mkitumia njia nyingi za kiutendaji, shughuli za mikono katika hatua za awali ili waweze kujenga taswira akilini ambayo itawawezesha kuelewa katika hatua za baadaye. Katika hatua hii, utapanga njia za kuwataarifu wanafunzi juu ya dhana ya uzito katika hatua hizi tatu:

kulinganisha uzito wa vitu viwili au zaidi kwa kuvibeba kwa wakati mmoja; kukadiria na kupima uzito wa vitu kwa kutumia vipimo visivyo sanifu kama mawe; kupima na kulinganisha uzito kwa kutumia vipimo sanifu.

Kitu muhimu katika kazi hii ni matumizi ya mizani zinazoweza kuundwa na vitu rahisi na vinavyopatikana (angalia Nyenzo rejea ya 1: mzani rahis i). Kwa ushauri jinsi ya kukusanya zana za kufundishia, angalia Nyenzo rejea Muhimu: Kuwa mwalimu mbunifu katika kukabili changamoto za mazingira.

Nyenzo rejea 4: Kipimo cha Mvua Dar es Salaam